Utayarishaji sahihi wa ardhi na udhibiti wa magugu husaidia kuongeza mavuno ya muhogo. Kulima, kuweka mitaro, pamoja na njia nyingine za usimamizi husaidia kuongeza mavuno ya muhogo.
Vaa vifaa vya kujikinga kila wakati unapotumia dawa za kuua magugu ili kuhakikisha usalama zaidi. Dawa za kuua magugu huwa na ufanisi wakati mimea ni ya kijani kibichi. Kuweka mitaro ni muhimu sana na vile vile huhifadhi maji ya udongo na kuchelewesha ukuaji wa magugu. Kulima hulegeza udongo, hudhibiti magugu, huwezesha mizizi kupenya na kuharakisha utoaji wa virutubisho kwenye nyenzo za kikaboni, na hivyo kuongeza mavuno.
Mbinu za kilimo
Wakati wa kupanda muhogo, chagua shamba lenye udongo wenye rutuba na unyevu kwenye mteremko tambarare kwa ukuaji mzuri wa mmea. Kata vichaka vilivyo shambani ikiwa viko juu ya urefu wa 50cm. Lakini ikiwa viko chini ya urefu wa 50 cm, weka dawa za kuulia magugu. Pia nyunyiza dawa za kuua magugu wakati mimea ni ya kijani kibichi. Palilia wiki 2 baada ya kuweka dawa ya kuua magugu. Lima ardhi mara mbili ili kulainisha udongo, kudhibiti magugu, kuwezesha kupenya kwa mizizi, kuongeza kasi ya kutolewa kwa virutubisho kwenye nyenzo za kikaboni, na kuongeza mavuno.
Udhibiti wa magugu
Baada ya mvua kunyesha, panda kwa mita 1 kati ya safu na mita 0.8 ndani ya safu ili kupata msongamano bora wa upandaji kwa ekari. Nyunyizia dawa za kuua magugu kwa usahihi ndani ya masaa 24. Tembelea shamba mara kwa mara ili kujaza pengo kwenye sehemu ambapo vipandikizi haviijaota. Palilia shamba ili kupunguza ushindani wa mwanga wa jua, maji na virutubisho, na hivyo kuongeza ukuaji mazao, na mavuno.