Homa ya mafua ya ndege huambukizwa sana na huathiri mfumo wa upumuaji, mfumo wa usagaji chakula na mfumo wa mishipa ya fahamu, na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi.
Virusi vya mafua ya ndege ni huathiriwa sana na sabuni na viuaviini. Virusi hivyo pia hupoteza uwezo wavyo wa kuambukia baada ya dakika 15 vikiwekwa kwenye halijoto ya digrii 56, na huuawa baada ya dakika 1 tu vikiwekwa kwenye halijoto ya digrii 100. Mafua ya ndege huathiri kuku, bata mzinga, bata bukini na aina nyingi za ndege wa mwituni lakini ndege wa majini hustahimili mafua ya ndege. Kipindi cha kuambukizwa cha ugonjwa huo hutofautiana kutoka saa chache hadi siku chache kulingana na aina, na kipimo cha virusi, njia ya kuambukizwa na umri wa ndege.
Biolojia ya ugonjwa
Ndege wa mwituni na bata wanaofugwa ni hifadhi asilia ya homa ya mafua ya ndege na hubeba virusi kwenye njia ya utumbo na huupitishia kwenye kinyesi. Virusi huenezwa kwa ndege wengine kwa kuvuta pumzi yenye chembechembe za virusi kutoka kwa makamasi pamoja na kupitia kugusana na kinyesi cha ndege walioambukizwa. Malisho yaliyochafuliwa, maji ya kunywa, vifaa, njia za usafirishaji wa malisho, trei za mayai na watu waliobeba virusi kwenye nguo na viatu vyao pia zinaweza kuwa njia nyingine ya kuenea kwa ugonjwa.
Ugonjwa hujidhihirisha katika aina mbili. Homa ya mafua ya ndege ya chini, ambayo husababisha dalili zisizo kali kama vile manyoya mabaya, kupungua kwa uzalishaji wa mayai na vifo vichache, huku mafua kali ya ndege yanaweza kusababisha vifo vingi sana.
Dalili na usimamizi
Dalili za kimatibabu ni pamoja na uvimbe wa kichwa na shingo, undu na kunyanzi pia vinaweza kuvimba na kuwa rangi ya bluu. Dalili za kupumua kama vile kukohoa na kupiga chafya, uvimbe mwa puani na makamasi, kuhara umaji. Dalili mfumo wa mishipa ya fahamu ni pamoja na kama vile kupinda shingo na kuyumbayumba, uvimbe kope za chini za macho, na macho kutoa majimaji, kutokwa na damu kwenye eneo la ngozi lisilo na manyoya haswa miguu ambayo ina rangi nyekundu isiyokolea iliyochanganywa na rangi ya buluu. Katika kuku wa mayai, ndege walioathirika wanaweza kutaga mayai yenye maganda laini na kisha kuacha kutaga kabisa.
Hakuna matibabu kwa ndege walioathirika lakini tunaweza kuzuia mashamba yetu kupata ugonjwa kwa kutekeleza mbinu sahihi za udhibiti wa kiasili, kuepuka kuwasiliana moja kwa moja na ndege wa porini, kuondoa uchafu, kuua viini bandani na kusafisha vifaa vyote, kuchanja vifaranga dhidi ya mafua ya ndege.