Kuku wa kienyeji au walioboreshwa wanaweza kufugwa popote nchini Kenya. Unachohitaji ni, wazo ka kibiashara, kujitolea na mtaji kidogo.
Kufuga kuku wa Kienyeji
Wafugaji wa kuku wa Kienyeji hufuga ndege kwa njia huria ambapo hakuna shughuli nyingi sana kwa za kutengenezea banda, kununua vifaa, kuwachanja na kuwatibu kuku.
Unapofuga kuku wa kienyeji zingatia kutengeneza banda lifaalo, mahali ambapo maji na malisho yatatoka, ufikiaji wa daktari wa mifugo na mahali utakapouza bidhaa zako.
Kuku wa Kienyeji ni sugu kwa magonjwa.
Aina za kuku wa kienyeji
Aina ya kari iliyoboreshwa huzalisha nyama na mayai kwa wingi, na kustahimili hali tofauti za hewa.
Aina ya kuroiler hujitafutia chakula, na huhitaji gharama nafuu za usimamizi.
Kuku aina ya upinde wa mvua hutoa mayai na nyama. Rangi yake ni bora sana. Aina hii haihitajiki sana, kwani hula sana. Aina ya Kenbro hutoa nyama na mayai na huupata uzito haraka.
Changamoto
Vifaranga hushambuliwa sana na maambukizi. Chakula cha vifaranga kisicho kizuri katika hatua ya kuwashughulikia kinaweza kuathiri ukuaji wa vifaranga.
Ukosefu taarifa sahihi huamua faida na hasara ya mradi. Unapojengbanda unapaswa kuzingatia uingizaji mzuri wa hewa, mwanga wa asili na nafasi ifaayo.
Chakula cha kuku
Katika mwezi wa tatu, lisha vifaranga mboga za majani ili kuongeza ubora wa nyama na mayai.
Chakula cha vifaranga kinapendekezwa kwa wiki nane za kwanza. Chakula cha kuku wa kienyeji wanaokua kinapendekezwa kutoka wiki ya 9 hadi karibu na juma la 16.
Chakula cha kuku wa kienyeji wa mayai kinapendekezwa kwa ndege wanaotaga mayai.