»Jinsi ninavyoongeza faida katika ufugaji wa kuku wa nyama«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=sFoP2EnytmI&t=328s

Muda: 

00:13:50
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

AIM Agriculture

Wafugaji wengi wa kuku wa nyama hupata faida kidogo. Faida inaweza kuongezwa kwa kutekeleza mbinu bora za usimamizi.

Kushughulikia takataka au matandiko ni kipengele muhimu sana katika ufugaji wa kuku na nguruwe kwa sababu ni mazingira ambayo ndege hulishia, hunywea na kulala. Hakikisha kwamba matandiko ni mazuri kwa ndege. Hii hufanywa kwa kuhakikisha kuwa matandiko au takataka ni kavu kila wakati. Kwa hivyo, weka vihori vya maji kwenye urefu unaofaa ili kuzuia ndege kumwaga maji kwenye sakafu wakati wa kunywa. Takataka zinaweza kuwa nyasi zilizokatwakatwa au maranda ya mbao.

Mbinu bora za kutunza kuku wa nyama

Dumisha uingizaji mzuri wa hewa kwenye banda la kuku ili kuruhusu gesi ya amonia kutoka ambayo husababisha matatizo ya kupumua kwa ndege.

Hifadhi idadi ya kuku inayopendekezwa, yaani wa kuku 12 kwa kila mita 2 ikiwa kuna banda wazi.

Daima geuza matandiko mara kwa mara, na weka safu nene ya matandiko wakati wa kuyabadilisha ili kuhakikisha kwamba inanyonya unyevu kutoka kwenye sakafu.

Utunzaji duni wa matandiko

Ikiwa hutatunza matandiko kuku wako watavamiwa na ugonjwa wa ngozi wa mguu, ambapo miguu hupata vidonda. Vidonda ni chungu na njia zinanzopitisha magonjwa. Matandiko yenye unyevu husababisha magonjwa mengine ya kuku.

Kwa kuwa vidonda vina uchungu, kuku hushindwa kutembea ili kuenda kula na kunywa, na hivyo basi hawezi kuongezeka uzito. Kuku hulazimika kulalia titi na kusababisha majeraha kwenye titi na hivyo kushusha ubora wa nyama.

Usimamizi duni wa matandiko pia husababisha mkusanyiko wa gesi ya amonia. Kiasi cha amonia kinaweza kupimwa kwa kutumia kifaa maalum na haipaswi kuzidi sehemu 5 kwa kila milioni.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0002:20Kushughulikia takataka au matandiko ni kipengele muhimu sana katika ufugaji wa kuku
02:2103:42Hakikisha kwamba matandiko ni mazuri kwa ndege kwa kutumia maranda ya mbao au manyasi.
03:4304:33Dumisha uingizaji mzuri wa hewa kwenye banda la kuku.
04:3404:55Hifadhi idadi ya kuku inayopendekezwa.
04:5607:52Ikiwa hutatunza matandiko kuku watapata ugonjwa wa ngozi wa mguu.
07:5310:25Usimamizi duni wa matandiko pia husababisha mkusanyiko wa gesi ya amonia
10:2612:10Matandiko yenye unyevu husababisha magonjwa mengine ya kuku.
12:1113:18Daima geuza matandiko mara kwa mara, na weka safu nene ya matandiko.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *