Jinsi Shamba la Sychar lilivyoongeza uzalishaji wao wa maziwa mara mbili katika miezi miwili – Sehemu ya 1

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=xmBchkMY4bE&list=RDCMUCZfzFgmReSD09S2L-cvg8uA&index=10

Muda: 

00:11:07
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Farm Kenya
Kuongezeka uzalishaji wa maziwa ya ng‘ombe maradufu kunaweza kufanywa ndani ya miezi miwili kwa kufuata utaratibu sahihi. Kulisha ng‘ombe kwenye silaji huboresha suala la uzalishaji wa maziwa.
Mbinu mbalimbali zimebuniwa na wakulima ili kuongeza uzalishaji wa maziwa. Mbinu hizo hutegemea eneo, upatikanaji wa malisho, na mfumo ufugaji unaotumiwa. Kabla ya kuanzisha ufugaji wa ng‘ombe wa maziwa, mambo yafuatayo yazingatiwe: Kwanza ni ardhi na pili ni vibarua kwa vile vibarua ni suala muhimu katika uzalishaji wa maziwa. Mwisho, mtaji ni muhimu ili kupata vifaa na kujenzi wa zizi la ng‘ombe.

Uchachushaji wa nyasi

Uchachushaji hufanywa kwa kutumia molasi kwani husaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa. Molasi ni muhimu kwa vile hutoa sukari kwa wanyama wa maziwa, huboresha ladha ya malisho na hutumika katika kutengeneza silaji ili kuhimiza uchachushaji. Pia hurahisisha mmeng‘enyo wa malisho.
Ili kuchachusha nyasi, kwanza zitandaze na kunyunyizia maji ili kuzilainisha. Molalasi huchanganywa na maji kwa uwiano wa 1: 1 na kunyunyiziwa juu ya nyasi. Kisha mchanganyiko wa nyasi huwekwa kwenye pipa na kushinikizwa.

Uhifadhi wa nyasi

Nyasi huhifadhiwa kwa muda wa siku 3–4 kwenye kifaa kisichopenyeza hewa ili kuruhusu uchachushaji. Lisha ng’ombe kwanza, na kisha umtolee nyasi zilizochachushwa. Katika mfumo wa kufugia wanyama ndani mtolee kila ng‘ombe anayekamua ni kilo 30 za silaji.
Uhifadhi wa silaji huhakikisha kuwa kuna uzalishaji wa maziwa mara kwa mara katika misimu yote ya kiangazi au ya mvua, na hivyo wakulima wanaweza kupata faida nzuri.

Kutolea wanyama dawa ya kuua minyoo

Dawa ya kwanza ya minyoo inapaswa kutolewa wakati mnyama ana miezi 2–4 au wastani wa miezi 3. Vipindi vya kudhibit minyoo hutegemea dawa iliyotumiwa. Kwa ng‘ombe wanaonyonyesha, watolee dawa mara moja kwani inabidi ungojee hadi saa 48 ili upate maziwa.
Ndama hutolewa dawa ya minyoo kila mwezi. Kwa jumla, baada ya kutolea ng’ombe dawa ya minyoo, ng‘ombe hukaa hadi masaa 72.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:14Kuongeza uzalishaji wa maziwa ya ng‘ombe maradufu ndani ya miezi miwili.
01:1502:45Umuhimu wa molasi kwa ng‘ombe wa maziwa.
02:4603:18Mbinu zinazotengenezwa na wakulima zinategemea eneo, upatikanaji wa malisho na mfumo wanaotumia.
03:1904:49Mchakato wa kuchchusa nyasi
04:5005:51Uhifadhi wa nyasi.
05:5207:22Mambo ya kuzingatia wakati au kabla ya kufanya ufugaji wa ng‘ombe wa maziwa.
07:2308:27Kulisha ng‘ombe silaji huongeza uzalishaji wa maziwa.
08:2809:36Mambo yanayosaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa.
09:3711:07Dawa za minyoo.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *