»Jinsi ya kuandaa shamba la migomba kwa mavuno bora«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=_w01x1idINc

Muda: 

00:15:19
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Forever Gardens Limited

Migomba hulimwa sana, na mara nyingi huliwa kama kitindamlo. Uandaji t mzuri wa shamba wakati wa upandaji ni muhimu ili kupata mavuno bora.

Katika utayarishaji wa shamba, fyeka vichaka na uache baadhi ya miti ili ifanye kama vizuizi vya upepo kunapokuwa na hali mbaya ya hewa. Acha manyasi yakauke na kisha uyachome. Ardhi ambayo haijawahi kulimwa awali ina rutuba ya kiasili, na hivyo hakuna haja ya kuweka samadi wakati wa kupanda.

Usimamizi wa migomba

Anzisha shamba lako la migomba katika eneo lililo karibu na chanzo cha maji ili uwe na maji ya umwagiliaji endapo kutakuwa na haja. Ikiwa eneo hilo lina maji ya ziada, chimba mifereji ya maji shambani. Hii huzuia mafuriko ya shamba.

Miezi mitatu baada ya kupanda, weka samadi ya kuku ili kutoa virutubisho.

Ondoa machipukizi ya migomba ya ziadi ili kuzuia ushindani wa maji na virutubisho unaosababisha mimea kudumaa. Machipukizi ya migomba yaliyoondolewa yanaweza kupandwa mahali pengine na hivyo kuongeza idadi ya migomba.

Ikiwa una pesa walaki hauna muda, unaweza kuwekeza katika kilimo kupitia makampuni yanayoaminika. Haya yanaweza kukusaidia katika usimamizi wa shamba lako.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:55Katika utayarishaji wa shamba, fyeka vichaka na uache baadhi ya miti ili ifanye kama vizuizi vya upepo.
00:5601:35Acha manyasi yakauke na kisha uyachome.
01:3602:23Ardhi ambayo haijawahi kulimwa awali ina rutuba ya kiasili, na hivyo hakuna haja ya kuweka samadi wakati wa kupanda.
02:2402:55Anzisha shamba lako la migomba karibu na chanzo cha maji
02:5604:35Ikiwa eneo hilo lina maji ya ziada, chimba mifereji ya maji shambani.
04:3609:45Miezi mitatu baada ya kupanda, weka samadi ya kuku, na ondoa machipukizi ya migomba ya ziadi ili kuzuia ushindani wa maji na virutubisho.
09:4615:10Unaweza kuwekeza katika kilimo kupitia makampuni yanayoaminika.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *