Kabla ya kuanza biashara ya ufugaji wa nguruwe, kuna mambo ya kimsingi ambayo unapaswa kuyazingatia.
Ili kuanza ufugaji wa nguruwe, unahitaji ardhi lakini kwa kuwa watu hawapendi kuishi karibu nguruwe, tafuta sehemu iliyo mbali na makazi. Jenga chumba kilicho na kivuli, paa na zizi zenye ukubwa tofauti. Mazizi madogo ni ya nguruwe mmoja huku mazizi makubwa yakihifadhi nguruwe wengi.
Mambo mengine ya kuzingatia
Maji ni muhimu. Ni bora kuwa na kisima kwa sababu huwezi kuendesha ufugaji wa nguruwe kwa kununua maji.
Ikiwezekana, kuwa na malazi ya wafanyakazi wako karibu na mabanda ya nguruwe ili waweze kushughulikia wanyama ipaswavyo.
Nguruwe ni walaji wazuri wa aina mbalimbali za chakula. Unaweza kuwalisha kwa taka kama vile taka kutoka kwa kiwanda cha kutengenezia pombe, taka za jikoni kama maganda na taka za mboga kutoka sokoni.
Nguruwe huzaa watoto wengi, na huwa na muda wa ujauzito wa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Baada ya kujifungua, unaweza kuwanyonyeshe watoto wa nguruwe kwa muda wa wiki 4 na kuwaachisha baadaye.
Soko la nguruwe limegawanywa. Unaweza kuuza baada ya kuwaachisha kunyonya. Waweza pia kuuza nguruwe waliokomaa au nyama ya nguruwe.