Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa kanga hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.
Kanga ni ndege wenye yenye faida kubwa, bidhaa zao zina mahitaji makubwa sokoni na ufugaji wao ni rahisi. Kanga ni ndege sugu ambao hustahimili magonjwa, na hutoa bidhaa bora kama vile mayai na nyama.
Usimamizi wa kanga
Ufugaji wa kanga kibiashara una faida, na ni chanzo kizuri cha ajira, kunahitaji ardhi kidogo ukilinganishwa na ufugaji wa ndege wengine. Ingawa kanga hupenda kujilisha wenyewe, jenga banda ili kuwalinda dhidi ya mvua, jua na wanyama wawindaji.
Weka kila ndege katika eneo la muachano wa futi 2–3 za mraba ili kupunguza mafadhaiko. Tandika sakafu na matandiko ambayo yanaweza kufyonza unyevu, vile nyasi zilizokatwakatwa. Matandiko yanaweza kudumu na kutumika kwa miezi saba ikiwa yatatunzwa makavu. Weka kanga katika banda safi.
Usifungie kanga jogoo na kuku jogoo katika banda hilo hilo, kwani kanga jogoo atakimbiza kuku jogoo mbali na chakula na maji. Fungia kanga ndani ya banda kila siku ili waweze kutaga ndani badili ya kutaga kwenye viota vilivyofichwa nje. Nunua kanga baada ya kujenga banda.
Kanga hupenda njia huria ya ufugaji na wanaweza kukidhi mahitaji ya lishe peke yao, na kwa ujumla hula wadudu, viwavi na majani. Hakikisha kuna mboga za majani na magamba ya konokono. Ikiwa ndege wamefungiwa ndani, wape chakula cha madukani na chakula cha nyongeza.
Hatimaye, kanga ni ndege sugu ambao hustahimili magonjwa.