Ili kuongeza tija ya michikichi, unahitaji kutekeleza mbinu bora za usimamizi wa shamba.
Kabla ya kuanzisha bustani ya michikichi, hakikisha kwamba unachanganua udongo ifaavyo na lazima eneo liwe na upenyaji mzuri wa mwanga wa jua pamoja na unyevu wa kutosha. Ili kuanzisha uzalishaji wa mafuta ya mawese, pata mbegu zilizoboreshwa na utengeneze kitalu. Hizi huanza kutoa matunda kati ya miaka 3 hadi 4. Mbegu ambazo hazijaboreshwa huchukua kati ya miaka 6 hadi 7 kuanza kuzaa matunda.
Kupandikiza
Baada ya miezi 6, pandikiza miche shambani kuu. Wakati wa kupandikiza, chimba mashimo ya kupandia huku ukitenganisha udongo wa juu na wa chini.
Jaza shimo na udongo wa juu ili kufanya kama msingi wa mmea. Ondoa karatasi ya plastiki kwenye mche na uupande kwenye shimo. Usipande mche kwa kina kirefu sana kwenye shimo kwa sababu huku kunaweza kupunguza ukuaji.
Ikiwa kuna wadudu waharibifu katika eneo hilo, tumia waya kulinda miche kwa angalau mwaka mmoja.
Usimamizi
Baada ya kuota mizizi (takriban siku 30 baada ya kupandikiza), ongeza mbolea ya urea ili kuhimiza ukuaji wa mimea.
Palilia shamba kwa kutumia dawa za kuua magugu au kwa mikono. Kama huwezi kupalilia shamba lote, palilia angalau nusu mita kuzunguka mmea. Huku kunaweza kupunguza ushindani wa mimea na magugu kwa virutubisho na maji.
Wakati mchikichi umezeeka na hautoi tena matunda ya kutosha, kata mti huo na upande mche mpya.