Maji moyo ni moja wapo ya magonjwa ambayo yanaweza kusababisha hasara kubwa katika ufugaji wa mbuzi.
Kuna magonjwa mengi ya mbuzi, ambayo mengine yanaweza kudhibitiwa wakati mengine huja kama milipuko. Yanakuja ndani ya muda mfupi na husababisha vifo vya wanyama wengi. Kifo cha ghafla cha mnyama kinaweza kuhusishwa na sumu au maji moyo. Wanyama wenye ugonjwa wa maji moyo hawaonyeshi dalili za kiafya yaani mnyama huamka akiwa mzima na mwenye afya njema kisha hufa ghafla au mnyama hutoka nyumbani akiwa mzima na kisha hufa ghafla shambani.
Dalili za ugonjwa wa maji moyo
Mnyama aliyeathiriwa na maji ya moyo huanza kutoa mate mdomoni, huanza kuyumbayumba akitembea, na kutokwa povu mdomoni katika kifo, hurusha mateke wakati wa kufa na pia hunyoosha shingo wakati wa kufa.
Maji ya moyo huleta maji moyoni na kufanya moyo kushindwa kusukuma damu. Ugonjwa huo unaweza kuua sana wanyama wachanga kutokana na kingamwili zao duni.
Udhibiti
Katika matukio ya ugonjwa wa maji moyo, watolee wanyama wako wote dawa za kuua viini ili kuzuia vijidudu kuzidi mwilini.
Nyunyizia dawa vizuri na uendelee kutumia viuatilifu vyenye viambato tofauti ili kuzuia kupe kupata upinzani dhidi ya viuatilifu fulani. Hakikisha unachanganya kipimo sahihi cha viuatilifu, nyunyuzia dawa na ogesha wanyama wote.
Ikiwa unashukia kuwa kuna ugonjwa wa maji moyo katika kundi lako, wape wanyama dawa ya oxytetracycline, na fuata ratiba yako ya kunyunyizia dawa.