Mdondo au kideri ni ugonjwa wa virusi ambao unaweza tu kudhibitiwa na si kutibiwa. Ugonjwa wa mdondo unaweza kudhibitiwa kwa kuwachanja ndege katika hatua tofauti.
Kuna aina mbili za chanjo: chanjo ya mdomoni, na chanjo ya lasota. Unapotumia chanjo ya mdomoni, changanya kipimo kwa kuvunja kifuniko cha chupa huku ukifungulia chanjo ndani ya maji. Tumia maji ambayo hayana klorini kwa ufanisi mzuri wa chanjo.
Chanjo ya Lasota
Chanjo ya Lasota hudungwa kwa kuku na hufanya kwa miezi sita bila ugonjwa wa kideri kutokea tena. Ili kuhifadhi chanjo kwa muda mrefu, weka chanjo kwenye jokofu, lakini usiigandishe.
Jinsi za kuchanja ndege
Unaweza kutumia sindano ya kawaida au sindano ya kiotomatiki.
Unapotumia sindano ya kiotomatiki, ingiza sindano ndani ya chupa ua chanjo, uiunganishe na kifaa cha ya kuchanjia. Tumia sindano ndogo kutoboa sehemu ya juu ya chupa ya chanjo ili kupitisha hewa.
Chukua sindano ambayo haijatumiwa na uifunge kwa ncha ya kifaa cha kuchanjia, na usome kipimo kabla ya kutumizi chanjo.
Sehemu za kudunga chanjo
Usimwage chanjo kwenye sakafu ili kuzuia kuenea kwa sehemu zingine za shamba. Unaweza kudunga ndege sindano katika sehemu mbili; matiti na mapaja. Dunga sindano kwa muinamo wa digrii 60, huku ukiepuka ncha ya sindano kugusa mfupa.
Unapomshikilia ndege wakati wa kumchanja, shikilia miguu kwa nguvu na utumie mkono wa kushoto kumshika ndege kwa mabega ili kuhisi sehemu ya matiti utakayodunga.