Kabla ya kuvuna, wakulima wengi hawajui ni kiasi gani wanachoweza kupata kutoka kwa mashamba yao. Kujua hii husaidia mkulima kupanga vizuri.
Ili kukadiria thamani ya mazao, wakulima wanahitaji kupima shamba kwa kujua idadi ya mimea iliyo shambani . Anza na kupata ramani sahihi ya shamba, kisha upime ukubwa wa shamba, na idadi ya mizizi ya muhogo inayotarajiwa kutoka shambani. Masuala yanayosababisha mavuno ni pamoja na: aina ya udongo, mkao wa shamba, aina ya mbegu, na usimamizi wa mazao.
Sampuli za mihogo
Hesabu idadi ya mimea ya mihogo kwa kila kipimo, na kiasi kinachozaliwa kwa kila mmea. Chagua maeneo 3 ambao yapo mbali na mipaka ya shamba. Unda umbo la pembetatu: Shikilia ncha ya kila kamba kwa kijiti, na hakikisha kwamba umbo hilo litakua na mita 5 kila upande. Vuna mimea 3 iliyokaribu na kila kona ya pembetatu. Kata mizizi yote kwenye shina na uondoe udongo pia. Ncha ya mzizi pia inakatwa pande ambapo kipenyo ni 1.5 cm, kisha sajili idadi na uzani wa mizizi safi.
Kuhesabu mavuno
Kwa kutumia programu ya simu: Pima ukubwa wa shamba, chagua sehemu 3 zinazowakilisha shamba lote. Kisha pima umbo la pembetatu katika kila eneo. Hesabu idadi ya mimea iliyo ndani ya kila umbo la pembetatu, na kisha vuna mihogo 3 iliyokaribu na kona 3. Pima uzani wa mizizi kwa kila mmea.
Kuhesabu mavuno / hekta: Idadi wastani ya mimea X uzito wa wastani wa mizizi kwa kila mmea / 10.826 (mita za mraba katika kila pembetatu / hekta).
Mazao / hekta X ukubwa wa shamba = mavuno ya shamba.
Mazao ya shamba / 10.826 = mavuno ya wastani (kg / kilomita za mraba) / mavuno ya wastani (kg / kilomita za mraba) X 10.000 (idadi ya mita za mraba katika kila pembetatu) = Mazao kwa kila shamba.