Mtama ni mmea wa jamii ya nyasi inayokuzwa kwa ajili ya nafaka, ambayo pia husindikwa kuwa sharubati. Ukuzaji wake ni rahisi kama wa mahindi, ila tu mtama hustahimili ukame na mafuriko.
Aina mbalimbali za mtama hukomaa kwa nyakati tofauti, lakini aina nyingi huchukua muda wa siku 90 hadi 150. Aina za ubora wa juu zaidi hutoka kwenye mtama ambao huchukua siku 100 – 120 kukomaa. Muachano unafaa kuwa 75cm kati ya safu, na 20 cm ndani ya safu kwa aina zinazokomaa mapema, 25cm kwa aina za wastani na 30cm kwa aina zinazochelewa kukomaa
Kilimo cha mtama
Chagua eneo lenye udongo tifutifu ulio na kina kirefu, na hali joto ya hewa. Mtama huhitaji mvua kati ya 600mm – 1000mm kwa mwaka.
Andaa shamba kwa kutumia majembe, matrekta, ng‘ombe na dawa za kuua magugu.
Chagua aina bora ya mbegu kutoka kwa vyanzo vya mbegu vilivyoidhinishwa.
Wakati wa mvua, panda mbegu katika mistari na muachano wa kutosha. Awali, mbegu hizo zinafaa kupakwa na viuakuvu kama vile apron plus ili kudhibiti nzi.
Weka mbolea kwa umbali wa 6cm – 8cm kutoka kwenye mmea ili kuepuka kuunguza miche michanga.
Ongeza mbolea oza au samadi ili kukidhi mahitaji ya virutubisho vya udongo.
Dhibiti magugu kwa utayarishaji mzuri wa ardhi, hivyo palilia kwa mikono, nyunyiza dawa za magugu, zungusha mimea kwa kupanda mimea mitego kama vile pamba, na karanga.
Dhibiti wadudu na magonjwa wa mtama ili kuongeza mazao.
Vuna nafaka mara tu zinapokomaa, zikaushe vizuri, na zihifadhi. Pura na kutibu nafaka ili kudhibiti wadudu.