Mchicha ni mmea unaostahimili joto, una lishe kadhaa, huhitaji joto la udongo kati ya nyuzi joto 20–30 ili kustawi. Mchicha huchukuliwa kuwa zao la nafaka kwa sababu ya mbegu zake ndogo zenye ladha.
Mchicha unaweza kuvunwa ukiwa mchanga na kuongezwa kwenye mchanganyiko wa saladi. Majani yake makubwa na mashina yanaweza kutokoswa. Hata hivyo, uwekaji wa mbolea unapaswa kuwa wa wastani kulingana na aina ya mboga zitakazopandwa. Wakati mzuri wa kuongeza mbolea ni ule ambao dalili za upungufu wa madini zinapoonekana. Mbolea inapaswa kuwekwa kabla ya kutayarisha shamba ili kuwezesha usambazaji sahihi wa virutubisho kwenye udongo, na ufyonzaji sahihi wa madini.
Mahitaji ya kukuza mchicha
Kwanza chagua eneo ambalo hupata mwanga wa jua kwa masaa 6–8. Eneo lazima liwe karibu na chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji rahisi wakati wa kiangazi. Ongeza mbolea oza kwenye udongo pamoja na vyanzo vya nitrojeni kwa vile mchicha huhitaji nitrojeni zaidi ili kutoa majani zaidi. Hata hivyo, mbolea zisitumike kwa wingi kwani zinaweza kuathiri ukuaji wa mizizi.
Samadi ya wanyama huwekwa kwa vile hupatikana kwa gharama nafuu. Wakati wa kupanda, changanya na udongo wa kichanga na mbegu ili kuzitawanya vizuri kwa vile ni ndogo sana. Tawanya mbegu shambani kwa uangalifu na uzichanganye kwenye udongo. Hakuna haja ya kupanda katika safu. Mbegu zinapaswa kumwagiliwa maji kila wiki wakati wa ukame ili kuongeza viwango vya unyevu kwa uzalishaji bora.
Vuna kwa kukata mmea mzima inchi chache juu ya ardhi, siku 7 hadi 14 wakati mmea umechipua majani halisi ya kwanza. Acha mmea kufikia urefu wa futi 1 hadi 2 kabla ya kuvuna ili kupata mavuno bora.