Uanzishaji na usimamizi sahihi wa kitalu ni muhimu ili kuhakikisha uotaji bora wa mbegu.
Baada ya kupanda, mbegu huchukua siku 5 hadi 10 kuota. Iwapo asilimia 50 ya mbegu zimeota, ondoa matandazo kwenye kitalu na mwagilia maji. Uondoaji wa matandazo katika hatua hii huzuia uingiaji wa miche kwenye matandazo, jambo ambalo husababisha uharibifu wa miche wakati wa kuondoa matandazo.
Usimamizi wa kitalu
Siku moja hadi mbili baada ya kuondoa matandazo, nyunyizia viuakuvu kwenye miche ili kuzuia ukungu, na kisha endelea kunyunyizia dawa mara kwa mara baada ya muda maalum.
Siku nne baada ya kuondoa matandazo, weka mbolea ya majani, huku ukiongeza dawa ya kuua wadudu baada ya siku 5 hadi 7.
Wakati miche ina umri wa wiki 4, badilisha mbolea ya majani na uweke mbolea ambayo husaidia miche kustawi na kuwa migumu kwa ajili ya kupandikizwa.
Daima dhibiti magugu. Inashauriwa kutumia mikono kupalilia ili kutoathiri mizizi. Pia hakikisha kwamba sehemu ya juu ya kitalu imesawazishwa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Kupandikiza
Iwapo miche iko tayari kupandikizwa, lakini hakuna mvua wa kutosha, itolee miche virutubisho vidogo ili kupunguza kuaji.
Ikiwa ardhi yako ina mwinuko, tengeneza matuta bila kufwata mteremko ili kudhibiti mmomonyoko wa udongo.
Baada ya kupandikiza, dhibiti kwa makini magonjwa na wadudu waharibifu kama vile vidukari, chawa na utitiri.
Ikiwa udongo una fosforasi kidogo, ongeza Di ammoniamu phosphate wakati wa kupandikiza.