»Jinsi ya kulima mpunga, sehemu ya 2«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=JuyZsDRYVWE&t=92s

Muda: 

00:07:40
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

royaldreamtv

Mpunga ni zao la kibiashara na chakula ambalo hukuzwa ulimwenguni kote. Hata hivyo, ukuaji wake huhitaji hatua muhimu ambazo zikitekelezwa ipasavyo, mavuno mengi yanaweza kutolewa.

Kuna wadudu kadhaa wenye manufaa na wale wasio na manufaa katika mashamba ya mpunga. Miongoni mwa wadudu wasio na manufaa ambao huathiri zao la mpunga ni pamoja na mafunza, nzi weupe, viwavi jeshi n.k. Wadudu wenye manufaa ni pamoja na nyuki, kerengende na buibui, na wanapaswa kutunzwa shambani kwani wanafanya kama maadui asili wa wadudu waharibifu wa mpunga. Unapopanda mpunga, weka dawa za kuulia magugu kabla ya kupanda ili kudhibiti magugu.

Kupanda mpunga

Kila mara weka dawa za kuulia magugu siku 21 baada ya kupandikiza ili kudhibiti magugu. Hii huzuia magugu kustawi zaidi ya urefu wa mchele na hupunguza ushindani wa virutubishi na maji.

Vile vile, mwagilia kitalu ili kupunguza ukuaji wa magugu kwani mpunga hauwezi kustahimili ushindani huo. Hata hivyo, endapo kuna usimamizi duna wa maji shambani, tumia dawa zinazopendekezwa ili kukandamiza magugu.

Weka NPK kwa kiwango kinachopendekezwa siku 10 baada ya kupanda kwa sababu katika hatua hii, mizizi huwa imestawi vyema. Kwa upande mwingine, tumia urea katika hatua masuke ya mpunga yanapoinama ili kutoa gunzi bora. Unapoongeza NPK, kina kinapaswa kuwa 27cm kwani hii huzuia mbolea kuyeyuka.

Pia dhibiti wadudu waharibifu wa mpunga kwa kuchoma mabua, kulima na kufurika shamba baada ya kuvuna ili kukandamiza mabuu. Vile vile panda mseto na mahindi kwani huku kunapunguza mafunza shambani. Panda aina sugu za mpunga zinazostahimili magonjwa. Vuna siku 30–45 baada ya kuchanua maua wakati rangi ya mpunga kwenye masuki imebadilika kuwa njano au kahawia.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0002:37Kila mara weka dawa za kuulia magugu siku 21 baada ya kupandikiza ili kudhibiti magugu.
02:3802:53Mwagilia kitalu na hakikisha usimamizi mzuri wa maji shambani.
02:5403:05Endapo kuna usimamizi duna wa maji shambani, tumia dawa zinazopendekezwa ili kukandamiza magugu.
03:0605:18Weka NPK kwa kiwango kinachopendekezwa siku 10 baada ya kupanda.
05:1905:58Weka NPK kwa kina cha 27 cm. Ongeza urea kama inavyopendekezwa katika hatua ya kuchanua maua.
05:5906:28Weka mbolea karibu na shila la mmea wiki 1–2 baada ya kupanda na pia dhibiti wadudu
06:2906:53Panda mseto na mahindi na usiue wadudu wenye manufaa.
06:5407:19Panda aina sugu za mpunga. Vuna siku 30–45 baada ya kuchanua maua

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *