Maharagwe huongeza nitrojeni kwenye udongo na yana protini nyingi. Ukuaji wao unahitaji hatua chache, kwani maharagwe hupandwa moja kwa moja shambani.
Maharagwe huhitaji jua la kutosha, na udongo wenye unyevu na rutuba kwa ukuaji sahihi. Inashauriwa kuboresha pH ya udongo hadi 5.5–5.8 kwa kuongeza chokaa, kwani maharagwe huathiriwa na tindikali. Joto la udongo linapaswa kuwa 60–70 F kwa ukuaji sahihi. Acha umbali wa cm 10–15 kati ya mimea ni umbali wa 45cm kati ya safu. Loweka mbegu kwa saa 24 kabla ya kupanda ili kusaidia kuhimiza uotaji.
Hatua zinazozingatiwa
Anza kwa kuandaa shamba mapema, jaza mashimo na samadi iliyooza kwa ukuaji bora wa mmea.
Pia tengeneza mtaro wa mboji wenye kina cha sentimita 30 ambapo maharagwe yatapandwa na uujaze samadi ya wanyama ili kuongeza ukuaji. Panda mbegu safi, na ongeza viwango vya mbolea vilivyopendekezwa.
Maharage yanapofika mwezi 1, weka kilo 50 ya mbolea ya jasi kwa ekari ili kusaidia kutoa maganda, na naitrojeni.
Kisha chimba mashimo ya kupandia kwa kina cha cm 2.5–5, na panda mbegu 2–3 kwa kila shimo. Mwagilia mimea asubuhi ili kuzuia mnyauko na kudhibiti magonjwa ya ukungu. Acha umwagiliaji wakati asilimia 25% ya maganda ya maharagwe yamegeuka manjano.
Pia panda maharagwe pamoja na mahindi ili kulinda maua ya maharagwe wakati wa mvua. Katika hatua ya kuchanua maua, weka mbolea ya jasi kwa kiwango cha kilo 200 kwa kila hekta au samadi ya wanyama ili kuongeza mavuno.
Kila mara palilia shamba kwa mkono ili kuepuka kuharibu mizizi ya mimea, na kuvuna kwa wakati ufaao kulingana na aina ya maharagwe.
Pia weka mwarobaini au shaba kwa wakati ufaao ili kuzuia magonjwa ya ukungu, na fanya mzunguko wa mazao ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na mizizi. Epuka kufanya kazi shambani wakati majani yana unyevu ili kuzuia kueneza magonjwa ya ukungu na bakteria.
Mwishowe, kagua shamba kila mara ili kuangalia milipuko ya magonjwa.
Aina za maharagwe
Maharage ya kichaka; haya ni mafupi, hukua hadi urefu wa 60cm na hayahitaji vijiti vya kuhimili mmea.
Maharagwe aina ya pow, haya hukua hadi kufikia urefu wa mita 2.4– 3, huhitaji vijiti vya kuhimili mmea, ni rahisi kuvunwa na hutoa mavuno mengi. Aina zingine za maharagwe ni pamoja na maharagwe ya runners, maharagwe ya lima, mbaazi na maharagwe ya soya.