Malenge ni moja wapo ya mimea muhimu zaidi kwa sababu mbegu zake ni vyanzo vya zinki na chuma.
Ukuaji wa malenge huathiriwa sana na mbinu duni za kilimo.
Uzalishaji wake unategemea na aina iliyochaguliwa, msimu wa kupandia, na jinsi ya kupanda.
Kukuza malenge
Toa nafasi ya kutosha ili kuwezesha mimea kutambaa, pamoja na kuingiza hewa na mwanga wa jua. Tawanya 60g za mbolea ya NPK na kilo 3 za mbolea ya kikaboni kwa kila mita 2 kwenye kitalu. Andaa miche kwa idadi ya mimea 24000 kwa hekta huku ukiweka mbegu 1 kwa kila shimo.
Funika miche na udongo laini, mwagilia maji na weka trei kwenye kitalu kilicho na unyevu wa kutosha na hewa. Baada ya siku 8 hadi 10 ondoa kivuli na punguza umwagiliaji wa maji ili kufanya miche iwe na nguvu, na kisha uandae mashimo ya kupandikiza.
Wakati wa kupandikiza, miche yenye mizizi iliyostawi vizuri huwekwa kwenye mashimo yaliyotayarishwa kwa kina kinachofaa, na umbali wa mita 1.5 kutoka mmea mmoja hadi mwingine kutegemea aina na msimu. Mwagilia maji baada ya kupandikiza na ukague mimea mara kwa mara ili kuzuia magonjwa yasienee.
Endelea kuweka mbolea juu ya mizizi mara kwa mara huku ukifuata mapendekezo. Mwagilia maji mara kwa mara na fanya mashauriano.
Kuvuna malenge
Malenge huvunwa siku 70 – 90 baada ya kupandikiza kutegemea na aina. Wakati bora wa kuvuna ni asubuhi na alasiri. Malenge yaliyovunwa huwekwa kwenye eneo lenye kivuli na hewa ya kutosha.