Pilipili hukuzwa kwenye aina kadhaa za udongo kwa njia za usimamizi zinazofaa.
Kuna aina kadhaa za pilipili, kila moja ikiwa na sifa zake kwa mfano Trinidad scorpion; ambayo ni moja ya aina kali zaidi. Pilipili hoho; hii ina rangi tofauti. Pilipili aina ya cayenne, ambayo huhifadhiwa kwa urahisi katika hali ya unga. Magonjwa makuu ya pilipili ni pamoja na; bakadoa, chule, bakajani, kuoza kwa shina, batobato, vifundo vya mizizi. Wadudu ni pamoja na minyoo, nondo, vidukari, viwavi na mabuu.
Kupanda hadi kuvuna
Anza kwa kuchagua udongo wenye rutuba, unaohifadhi maji, ulio karibu na chanzo cha maji kwa kuwa pilipili huhitaji maji ya kutosha. Wakati wa kupanda, usitumie samadi mbichi kwa sababu hii huathiri uhifadhi wa mazao na ukomaavu.
Jenga kinga za upepo ili kulinda mimea dhidi ya upepo, kisha mwagilia miche vizuri wakati wa kupanda. Kupanda kunapaswa kufanywa wakati wa mchana ili mimea iweze kukua na nguvu zaidi usikukucha. Lakini katika hali ya hewa ya mawingu, upandaji lazima ufanyike asubuhi.
Jaza kila shimo la kupandia kwa lita 1 hadi 2 za maji ya vuguvugu na kisha panda mche kiwima. Daima mwagilia lita 1 hadi 2 ya maji kwa kila mmea kwa muda wa siku 2 hadi 3 ili mmea ustawi vyema. Mwagilia kila siku katika maeneo kavu na yenye joto.
Daima dhibiti wadudu na magonjwa kwa kutumia viuatilifu na kemikali zinazopendekezwa ili kuepuka hasara. Mwisho, vuna kwa wakati ufaao kulingana na mahitaji ya soko. Pilipili hoho inapaswa kuvunwa ikiwa haijakomaa kwani huharibika kwa urahisi.
Changamoto
Upungufu wa virutubishi vya udongo huleta changamoto, kwa mfano upungufu wa potasiamu husababisha majani kukauka. Upungufu wa naitrojeni husababisha majani kuwa na rangi ya kijivu. Upungufu wa magnesiamu husababisha majani kunyauka. Nitrojeni zaidi kupita kiasi hudondosha maua.