Mboga zinaweza kupandwa kutoka kwa vipandikizi. Mbinu hii inahitaji utaalamu. Mboga zilizopandikizwa vizuri huchukua siku 2 – 3 tu kutoa majani mapya na mizizi.
Iwapo unapandikiza mboga zenye mashina marefu, panda kwenye kina kirefu, na panda mboga zilizo na mashina fupi kwenye kina kifupi.
Kupandikiza mboga
Wakulima wanapaswa kupandikiza mboga wakati wa siku ya mawingu au alasiri ili miche ipate nguve tena kwa urahisi. Mwagilia miche ili iweze kunyonya maji ya kutosha, na pia kuwezesha udongo kushikilia vizuri mizizi. Tayarisha shamba kuu kwa kuongeza na kugeuza mboji au mabaki ya mimea ili iweze kuoza zaidi.
Chimbua miche kwa uangalifu ikiwa na udongo kwa mizizi. Tenganisha miche kwa upole. Ondoa nusu ya majani kutoka kwa mmea ili kupunguza kiwango cha uvukizi. Jaza pengo na mboga zinazokua kwa haraka ili kuongeza kipato. Mwagilia mimea kwa usawa ili kuhimiza ukuaji sahihi wa mizizi, na hivyo kuwezesha kunyonya virutubisho.