Ni matamanio ya kila mfugaji wa kuku wa nyama kufikia uzito unaohitajika kwa muda mfupi iwezekanavyo, lakini kuna baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuzuia hili.
Haya yanaweza kujumuisha kuzaliana duni, virutubishi duni na magonjwa. Inabidi udhibiti mambo haya ili kuwawezesha kuku wako kukua haraka. Chagua aina bora ya kuku kutoka kwa muuzaji anayeaminika; ukipata aina duni, juhudi zako zote za kuwa na kuku bora zitakua hasara. Tumia fursa ya siku saba za kwanza za maisha ya vifaranga yaani wape kiasi cha kutosha cha malisho kwa sababu uwiano wa ubadilishaji wa malisho ni wa juu zaidi katika hatua hii ya ukuaji. Kwa wiki za kwanza, lisha vifaranga na malisho ya kuanzia ambayo yana 23% ya protini. Wiki 4 hadi 8, wape chakula cha ukuaji ambacho kina asilimia 19% ya protini. Daima jaza vihori vya chakula na malisho, na kila wakati uwape maji mengi ya kunywa.
Hatua nyingine za usimamizi
Epuka kuwanyima vifaranga wako chakula na walishe libitum. Hii husababisha ukuaji bora.
Shughulikia banda lako la kuku. Watolee maji safi kila siku, pamoja na mwanga wa kutosha ili waweze kula vizuri, na pia kukagua banda mara kwa mara ili kuona dalili zozote za uharibifu na hivyo kuzuia wanyama wawindaji kuingia, na pia tolea vifaranga nafasi ya kutosha.
Wape vifaranga wako vichochezi asili vya ukuaji kama vile kitunguu saumu, pilipili na tangawizi. Hivyo pia hutumika kama viuavijasumu asili dhidi ya magonjwa.
Wekeza katika malisho bora. Nunua malisho ya kuku kutoka kwa muuzaji anayeaminika. Ukiona ukuaji wa polepole unapotumia malisho ya dukani, tolea kuku chakula kilichotengenezwa kutoka kwa mahindi, soya na damu.
Chambua kuku wako kulingana na ukubwa na uzito. Hii husaidia kufikia usawa katika ukuaji, na pia hudumisha afya ya kuku.