Kuna aina mbalimbali za minyoo ambao huozesha taka za kikaboni, na hutoa bidhaa ya mwisho inayoitwa mbolea ya minyoo.
Andaa kitalu ncha mbolea chenye upana wa 1m na urefu wa 5m. Ongeza taka za kikaboni. Mwagilia maji kwa kitalu ili kudumisha unyevu. Angalia kitalu mara kwa mara. Ongeza kilo 1 ya minyoo aina ya kiafrika katika kitalu. Minyoo hula takataka za kikaboni na kuipitisha kupitia mfumo wa usagaji chakula. Hii hutoa kinyesi kinayojulikana kama mbolea ya minyoo.
Hatua za kuzingatia na tahadhari
Minyoo hupenda hali ya giza. Funika juu ya kitalu cha mbolea, lakini hakikisha kwamba kuna uingizaji mzuri hewa mzuri. Unaweza kutumia magunia au nyenzo zozote zinazopatikana katika eneo lako.
Epuka kutumia karatasi za plastiki kwani zinaweza kuzuia joto na gesi. Unaweza kutengeneza kitalu kidogo kwa kutumia beseni. Hii hutumika kwa bustani ndogo za nyumbani.
Epuka vifaa vya mafuta na taka ambazo zinaweza kuvutia mchwa. Angalia kiwango cha unyevu mara kwa mara. Joto lingi huua minyoo, wakati maji mengi sana huwafukuza. Mbolea ya minyoo huwa tayari kuvunwa baada ya mwezi mmoja
Kuvuna na kutumia mbolea ya minyoo
Anzia juu ya kitalu kuvuna mbolea. Chuja mbolea iliyovunwa ili kutenganisha minyoo na nyenzo ambazo hazijaoza. Rudisha mabaki kwenye shimo kitalu cha mbolea.
Mbolea inaweza kutumika mara moja au kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Hakikisha unakausha mbolea kabla ya kuihifadhi. Mbolea ina kiasi kizuri cha virutubisho na madini ambavyo huhitajika kwa mimea. Mbolea inaweza kutumika katika njia kadhaa.