Nyasi aina za napia ni malisho bora kwa kutengeneza silaji (lishe lililohifadhiwa).
Nyasi za napia zimekithiri protini na wanga ambayo ni muhimu sana kwa ukuaji mzuri wa wanyama, na hivyo ni muhimu sana kwa kutengeneza silaji. Silaji hutengenezwa kwa kukushinikiza nyasi na kisha kuzifadhi. Huku kunaweza kufanywa na molasi au bila molasi.
Kutengeneza silaji
Ili kutengeneza silaji kutoka kwa nyasi za napia, ni vyema ukakata nyasi wakati zina takribani vifundo sita. Katika hatua hii, nyasi zinaweza kuchipuka tena baada ya kukatwa, na pia nyasi huwa zimepata nishati ya kutosha. Usivune nyasi ikiwa zimekua sana, kwani katika hatua hii, nyasi za nepia huwa ngumu sana na hazina ladha.
Wakati wa kutengeneza silaji kwa uso wa ardhi, tandaza chini damani ya plastiki na ukate nyasi katika vipande vidogo, na weka vipande hivyo kwenye damani ya plastika.
Shinikiza nyasi zilizokatwa kwa kuviringisha pipa iliyojazwa na maji juu yazo ili kuondoa hewa.
Funika juu ya silaji kwa kutumia damani ya plastiki nyingine na uongeze udongo.