Uuzaji wa chakula
Kwanza, kikundi cha wakulima wa kikaboni wanapaswa kuthibitisha bidhaa kupitia mfumo shirikishi wa dhamana na kuonyesha wateja wao cheti cha kilimo cha kikaboni. Pia wakulima wanapaswa kushiriki katika matangazo ya kila wiki ya vyakula vya asili na bidhaa za kikaboni na waanzishe huduma ya ugavi wa bidhaa za kikaboni kwa wateja.
Vile vile, tengeneza menyu ya bidhaa zinazopatikana na uzisambaze kwenye mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki, na uwaruhusu wateja kuagiza bidhaa wanazotaka. Siku moja kabla ya kupelekea wateja bidhaa, wanachama huvuna na kufungasha bidhaa zao za kikaboni, na wanachama wote huleta bidhaa zao safi asubuhi kwenye vituo vya kukusanyia ambapo bidhaa hufungashwa ili kupelekwa kwa kila wateja.
Wafunze wakulima kwa njia nyinginezo pia kwa kuandaa mipango ya elimu na burudani. Hatimaye, ungana na taasisi nyingine ili kukuza chakula cha kikaboni.