Kukata mashina ya mikahawa mara kwa mara na kupogoa matawi kila mwaka huongeza mazao na mapato.
Kata mashina ya miti mizee sana ambayo haizai vizuri, na iliyo na matawi mengi bila matinda ya kutosha. Hata hivyo, usikate mashina zaidi ya theluthi kwa wakati moja, kwa sababu hautopata mazao yoyote kwa mwaka mmoja baada ya kukata mashina. Kata katika shahada ya 45 ili kusababisha matawi 3 mapya kuota. Kata matawi kati ya 30–50 cm juu ya ardhi kwa ulaini ili kuzuia magonjwa. Baada ya mwaka mmoja, shamba litanawiri huku likiotesha majani mapya mengi.
Njia ya kupogoa
Kupogoa hufanywa mwishoni mwa mavuno makuu kwa kutoa matawi ambayo yalikuwa hayazai, na vile vile mkahawa huota matawi mapya. Tumia msumeno au mkasi mkali. Hakikisha kwamba mti una urefu wa mita 2 ili kurahisisha kuchuma na pia mashina yasizidi 4 kwani mashina mengi hupunguza uzalishaji.
Ondoa matawi ambayo hayajakaa vizuri, matawi ya pili na ya tatu kwa sababu haya hayatowi mazao mazuri na pia huchukua nguvu nyingi za miti.
Toa matawi mara kadhaa ili kupunguza ushindani wa virutubisho. Hakikisha kwamba unapogoa kwa sababu kunaongeza upenyezaji wa mwanga wa jua, nguvu na upitiaji mzuri wa hewa, na hivyo kupunguza unyevu na joto. Pia ondoa matawi yaliyokaribu na ardhi ili kuzuia magonjwa kuenea kwa urahisi. Mwishowe, zika au choma matawi yaliyo na magonjwa ili kupunguza kueneza magonjwa.