Ubora na wingi wa mazao kutoka shamba la kilimo huathiriwa sana na kiwango cha rutuba ya udongo.
Kwa vile mbolea za kemikali huchafua maji na ardhi, matumizi ya mara kwa mara ya mbolea za kemikali pia hufanya udongo kugandamana, hufanya magugu na mimea kukua kupita kiasi. Majani ya mazao huvutia wadudu.
Kichochezi asili cha ukuaji wa mazao
Vichochezi asili vya ukuzaji wa mazao hutumiwa kwa nafaka, mbogamboga na matunda, kusaidia katika uundaji wa maua, kuongeza ukubwa wa nafaka, huharakisha ukomavu wa mazao kwani mazao huvunwa siku 15 kabla ya ratiba.
Vile vile, kwa vichochezi asili vya ukuzaji wa mazao, changanya trei 1 ya samadi mbichi ya ng’ombe na 1/2 kg ya samli au siagi ili kuhimiza vijidudu vizuri kwenye kinyesi cha ng’ombe. Safirisha mchanganyiko kwenye chombo cha plastiki, ukifunike, na ukiweka kwenye kivuli, na baada ya siku 3 ongeza lita 10 ya mkojo na lita 10 ya maji na uuchanganye vizuri.
Funika chombo kwa kitambaa safi na ukoroge mchanganyiko asubuhi na jioni kwa dakika 10 kwa wiki 2 ili kuondoa gesi iliyobaki kwenye kinyesi cha ng’ombe. Baada ya wiki 2, ongeza lita 3 ya maji ya nazi, ongeza lita 3 ya maziwa safi na ongeza kwa upole lita 2 ya maziwa yaliyoganda na uchanganye vizuri.
Endelea kwa kuongeza kilo 3 za sukari ya asili ya kahawia ya molasi au ongeza ndizi 12 mbivu zilizopondwa vizuri kwenye mchanganyiko huo, na funika chombo na wavu au chandarua. Koroga mchanganyiko kila siku kwa wiki 2 ili viungo vyote vichanganyike vizuri.
Kusanya majani kutoka kwa mimea ya kienyeji yenye harufu kali ambayo mifugo hawali, na changanya kilo 1 ya majani kwenye lita 5 za mkojo, funika mchanganyiko kwa kitambaa safi na uweke kivulini kwa siku 10. Koroga mchanganyiko kila siku asubuhi na jioni.
Zaidi ya hayo, chuja dondoo ya majani mara 3-4 ili kuondoa chembe zozote, ongeza lita 1 ya dondoo iliyochujwa kwa lita 5 ya kichochezi cha ukuaji wa mmea na uweke mchanganyiko kwenye vyombo vilivyofunikwa kwenye kivuli kwa wiki 4. Loweka kilo 1 ya mbegu kwenye kilo 3 za mchanaganyiko kwa dakika 30 kisha zikaushe kwenye kivuli kwa saa 6 kabla ya kupanda. Kwa mmea unaoenezwa na vipandikizi, chovya mizizi kwa saa 1/2 kabla ya kupanda, na yeyusha lita 3 za mchanganyiko ndani ya lita100 ya maji ili kunyunyizia mboga na mtama.
Hatimaye, nyunyizia mimea wiki 2 baada ya kupandikiza na pia changanya vikombe 2 vya mchanganyiko kwa lita 20 za maji kwenye mfumo wa umwagiliaji wa matone.