»Kiini changu cha Kwanza – Kipindi cha 3 – Wakati sahihi wa Kuweka kitenga malkia katika mzinga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=ZM8XUrrZ4Zs

Muda: 

07:37:00
Imetengenezwa ndani: 
2023

Imetayarishwa na: 

Black Mountain Honey

»Kiini changu cha kwanza – Kipindi cha 3 – Wakati sahihi wa Kuweka kitenga malkia katika mzinga«

Unapomtambua nyuki-malkia na kugundua kuwa kila fremu ina kitu ndani yake, angalia iwapo kuna magonjwa ndani ya mzinga kabla ya kuweka kitenga malkia.
Kisha jiandae kwa kuvaa vazi maalu la kushughulikia nyuki. Tumia kifaa cha kutoa moshi ili kuondoa nyuki kabla ya kushughulikia ndani ya mzinga. Hakikisha kuwa halijoto halipo chini ya nyuzi joto 13 au 14 wakati unaposhughulikia mzinga. Pia, hakikisha kwamba unafanya ukaguzi wa mzinga kila wiki. 

Kuweka kitenga malkia

Jambo la kwanza unalotaka kuona kwenye bustani yako ya nyuki ni idadi kubwa ya nyuki vibarua ambapo takriban asilimia 80 ya fremu za mizinga iwe imefunikwa na nyuki.  
Katika mzinga wa unene wa fremu 10, unapogundua kuwa nyuki wamefunika takriban fremu 9 kwa wiki moja, ndipo hapo unapaswa kuweke kitenga malkia. Unapoweka kitenga malkia, hakikisha kuwa nyuki wote wameondolea kutoka juu ya fremu.

Udumishaji

Angalia fremu za mzinga moja baada ya nyingine ili kuona maendeleo yalipo kama vile uwepo wa mayai.
Iwapo haujaona ugonjwa wowote wakati anapokagua mzinga, basi weka kitenga malkia na pia ongeza juu yake kisanduku ambacho husaidia kuhifadhi asali ya ziada.
Tolea nyuki wako chakula cha kutosha. Kisha funika mzinga ipaswavyo.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:15Kagua nyenzo zilizo ndani ya mzinga
01:1602:05Angalia kama fremu za mzinga zimejazwa na mayai
02:0603:00Angalia iwapo takriban asilimia 80 ya fremu za mizinga iwe imefunikwa na nyuki.
03:0104:00Kushughulikia mzinga
04:0105:00Kagua uwepo wa ugaonjwa wowote ndani ya mzinga
05:0105:40Tumia kitenga malkia mbacho hugharimu bei nafuu
05:4106:40Angalia iwapo kuna nafasi ya kutosha ndani ya mzinga
06:4107:37Ongeza sanduku la ziada ili kupanua nafasi

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi