Kuunda kikundi na wakulima wengine kuna faida nyingi. Kila mtu anaweza kusaidia na pia kujifunza kitu.
Baadhi ya wakulima huhitaji mafunzo ili kujua kiasi gani wanaweza kuuza bidhaa zao. Kwa hivyo, wanapoteza pesa. Lakini Katika kikundi, wakulima wanaweza kujiunga pamoja na kushiriki maarifa na vifaa kati yao
Kufanya kazi katika kikundi
Katika vikundi vya kujisaidia kuna wakulima wachache ambao wanasaidiana na wanataka kupanua maarifa/ elemu yao. Wanakikundi huelezana kuhusu njia tofauti za usimamizi ambazo wanaweza kujisaidia nazo kwa ardhi yao, maoni mapya na watangulizi. Pamoja wanaweza kushughulikia changamoto zao.
Kikundi kinaweza kuamua sheria zao. Kwa hivyo ni muhimu kuzungumza juu ya nani anaweza kujiunga na kikundi cha msaada. Kwa mfano, munaweza kuamua kwamba mwanachama mpya anapaswa kuishi katika mahali fulani, anafanya kazi na kilimo cha uhifadhi au ni mtu mzuri anayejitihadi kufanya kazi kwa bidii. Wanachama pia wanaamua juu ya muundo wa kikundi. Kwa mfano unaweza kuchagua mwenyekiti, katibu, mweka hazina na maafisa wengine.
Katika kikundi munaweza kusaidiana kifedha. Kwa hivyo unaweza kuanza chama kidogo cha uhifadhi na mikopo. Kila wakati munakutana, kila mtu huleta pesa kidogo. Fedha hizi zinaweza kukopwa kwa wanakikundi kununua mbolea, mbegu au kulipia kazi. Mwanachama analipa pesa na riba.
Mara nyingi wakulima wana shida kuamua bei ya bidhaa zao. Wao huwa na kiasi tofauti cha bidhaa. Wanachama wanaweza kuweka mavuno yao pamoja na kuuza bidhaa kubwa kwa pesa zaidi.
Faida nyingine ni kwamba, unaweza kununua vifaa pamoja, ambavyo vingekuwa vya gharama kubwa kwa mkulima mmoja pekee. Kuna uwezekano pia wa kununua bidhaa kwa ununuzi mwingi ili kupata bei rahisi.
Watoa huduma na washirika wengine wanapenda kufanya kazi na vikundi, kwa sababu ni rahisi kwa serikali na mashirika mengine kufundisha na kujipanga na kikundi.