Ili kupanda mbaazi za kijani, unachohitaji ni mbegu, mbolea, dawa na kazi. Mbaazi zinapokaribia kuvunwa, zivune mara moja kwa sababu zikiachwa shambani kuna uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na majonjwa
Kilimo cha mbaazi za kijani
Baada ya kuvuna mbaazi changanya mabaki ya mazao kwenye udongo kabla ya kupanda zao linalofuata kwa sababu haya ni chanzo wadudu na magonjwa.
Baada ya kuandaa ardhi, tengeneza mashimo madogo shambani ambamo utapanda mbegu.
Ekari 1 takribani inahitaji kilo 20 za mbegu na kifuko kilo 50 za mbolea.
Baada ya hapo, unahitaji kunyunyizia dawa ili kuzuia wadudu kuathiri mbaazi.
palilia bustani huku ukiendelea kunyunyizia dawa.
Wakati wa kuchanua maua, weka mbolea ya majani yenye potasiamu na ongeza mbolea yenye kalsiamu wakati mmea unapoanza kutoa matunda.
Kwa wastani mbaazi huchukua miezi 3 kutoka kwa kupanda hadi kuvuna.
Changamoto kubwa katika ukuzaji wa mbaazi ni ugonjwa wa kutu ya majani ambao husababishwa na ukungu. Ugonjwa huo hudhibitiwa kwa kutumia dawa za kuua ukungu.
Visababishi vya mafanikio
Siri ya mafanikio katika kilimo cha mbaazi ni kutumia mbegu bora. Hata ukiwa na rasilimali nzuri kama mbolea lakini na ukatumia mbegu duni basi utashindwa.
Mzunguko wa mazao ni muhimu ili kuzuia wadudu na magonjwa.