Loweka mbegu kwa muda wa siku 3 hadi 5, badilisha maji kila siku na panda mbegu moja kwa shimo, lakini usipande chini sana.
Panda miche kwenye chumba cha wavu ili kulinda miche dhidi ya wadudu, na funika kwa damani ya plastiki endapo mvua kubwa itanyesha.
Hamisha miche kwenye kiriba cha palstiki siku 14 baada ya kupanda. Pandikiza miche kwa muachano wa sm 10 kwa 10. Miche huwa tayari kupandikizwa siku 45 baada ya kupanda.
Dumisha unyevu mara kwa mara siku nzima na uepuke kumwagilia jioni.
Maandalizi ya Ardhi na Kupandikiza
Udongo uliolimwa vizuri na vitalu vilivyoinuliwa husaidia kuhakikisha ukuaji wa mizizi yenye nguvu, na ukuaji wa mimea. Pia tengeneza mifereji ya maji ili kuzuia maji kutuama.
Andaa mashimo ya upanzi ya sm 10–15 yasiyo na kina kirefu na kupandikiza mimea alasiri.
Panda mpapai kwa muachano wa mita 2.5–3 kati ya safu, na mita 3m kati ya mimea, na mwagilia maji mara baada ya kupandikiza.
Kuhakikisha mavuno ya juu
Uwekaji wa mbolea hutegemea idadi ya mimea. Changanya dawa na unyunyuzie kwa uangalifu, vaa nguo za kujikinga na osha mikono vizuri baadaye na matumizi. Nyunyizia dawa ukizingatia muelekeo wa upepo ili kuepuka kukupeperushia dawa.
Ili huhakikisha mavuno mengi, lima udongo vizuri, panda miche yenye afya, acha nafasi sahihi, dumisha unyevu mzuri kwenye udongo, epuka kutuamisha maji shambani, hakikisha matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu.
Jua wadudu na magonjwa yanayoshambulia mipapai. Tumia mitego ya wadudu kupunguza idadi ya nzi wa matunda, ondoa matunda na mimea iliyoambukizwa, na dhibiti wadudu.
Shughuli za kuvuna
Matunda huwa tayari kuvunwa miezi 6–7 baada ya kupandikizwa. Uvunaji unaweza kufanywa kati ya 9 asubuhi hadi 3 jioni ili kupunguza mtiririko wa utomvu ambao unaweza kusababisha majeraha kwenye ngozi ya tunda.