Kilimo cha uyoga ni mojawapo ya aina za kilimo chenye faida zaidi. Uyoga ni chanzo kikubwa cha protini, na vitamini muhimu na una ladha.
Uyoga unaweza kukuzwa katika kila sehemu ya nchi. Utahitaji chumba cha kudumu ili kuunda mazingira mazuri kwa ukuzaji wa uyoga. Uyoga huhitaji unyevu na ulinzi dhidi ya hali mbaya ya hewa. Ukuzaji wa uyoga hautegemei mvua.
Chumba cha kukuzia uyoga
Tumia nyenzo za kienyeji zinazopatikana kama vile mbao na matope ili kuhifadhi unyevu. Jenga chumba cha futi 10 kwa 17, kwani halijoto linapaswa kuwa chini ya nyuzijoto 250 na kiwango cha unyevu kiwe 75c.
Kwa chumba cha mabati, unaweza kuweka dari kwa kutumia damani ya plastiki ili kudhibiti halijoto. Tandaza damani ya plastiki kwenye sakufu, na tandaza safu ya maranda ya mbao yaliyowekwa ndani ya maji. Funika madirisha kwa chandarua ili kuwezesha mzunguko mzuri wa hewa, na kuzuia wadudu kuingia. Usizuie mwanga wote kuingia.
Kutayarisha nyenzo
Ili kukuza uyoga, unahitaji nyenzo kama vile; makapi ya ngano, maganda ya mpunga, majani makavu ya migomba, maganda ya karanga, mabaki ya maharage au taka za kahawa. Jiandae kwa muda wa wiki 5 kabla ya kupanda mbegu za uyoga.
Endelea kumwagilia nyenzo maji. Katika siku ya nne, ongeza samadi ya kuku ili kutoa virutubisho vinavyohitajika kama vile nitrojeni. Acha nyenzo kwa siku 2 na uendelee kumwagilia maji. Ongeza mbolea ya urea ili kuongeza nitrojeni kwenye nyenzo. Hamisha msingi (nyenzo) kwenye eneo lenye kivuli ili zianze kuoza.
Mbegu za uyoga
Weka mifuko kwenye chumba kilicho na giza kwa muda wa siku 21. Mara tu mbegu zinapoanza kuota, ongeza takriban inchi 2 za udongo kwenye msingi.
Ikiwa uyoga una madoa unaweza kuwa umeathiriwa na ugonjwa wa ukungu au virusi. Nyunyiza maji kidogo mara tu zinapoanza kuenea, na zuia uchafuzi.
Vuna uyoga kwa mwezi mmoja na nusu. Baada ya kuvuna, safisha chumba na pia uua viini.