Kilimo msetu cha mahindi na mbaazi ni muhimu kuboresha thamani ya mahindi.
Mahindi huhitaji virutubisho vingi kutoka ardhini. Kila baada ya vuno, kiasi kadha cha virutubisho hivyo huondolewa ardhini. Baada ya kulima kwa myaka kadha, ardhi hupoteza rutuba nakadhalika, mahindi hukosa mavuno mazuri. Mahindi pia, hudumaa na huwa na rangi iliopauka yanapo kosa kupata virutubisho vya kutosha.
Mbaazi
Mbaazi husaidia kurejesha rutba ya ardhi, na pia huongeza nitrojeni ardhini kwa kuivuta kutoka hewani. Mizizi, mashina, na majani ya mimea huboresha udongo kwa kuongeza mbojo. Bora, mbaazi huendelea kunawiri hata kwenye kipindi cha kiangazi, kwasababu mizizi yao huvuta maji kuto chini kabisa ardhini.
Kilimo mseto cha mbaazi na mahindi
Kuna njia tele kadha za kulima mseto wa mbaazi na mahindi.
Kwa njia ya kwanza, tunapanda mbaazi kwa muachano wa 75 cm. Kisha, tunapanda mahindi katikati ya mimea miwili ya mbaazi.
Njia nyingine ni kwa kupanda mistari miwili ya mahindi ikifuatiwa na msatri mmoja wa mbaazi. Hakikisha kwamba kuna muachano wa 75 cm baina ya matuta, ili kusababisha uingizaji wa mwangaza wa jua wa kutosha. Matuta yanafaa kuwa juu ya 30cm. Katika misitari ya mbaazi, panda mbegu tatu nzuri kwa kila sehemu ya kupanda kwenye shimo ya kina cha 5cm. Katika mstari wa mahindi, panda mbegu moja nzuri baada kwa kila 25 cm. Hapo, mimea yatapata nafasi ya kutosha ili kuvuta virutubisho. Hakikisha kwamba unapanda mahindi na mbaazi katika siku moja ili mimea yote yaweza kupata manufaa ya mvua nyingi ya kuanza.
Njia ya tatu ni kwa kupanda mimea yote miwili kwenye tuta moja. Muachano kati ya mstari mmoja na mwengine ni 75 cm. Hapo basi, weka mbegu moja ya mahindi katika kila 25 cm. Pia, unapanda mbaazi katika kila sehemu ya tatu ya upanzi wa mahindi, na hivyo kuwa na muachano wa 75 cm kati ya mbaazi. Mwisho, panda mahindi kwenye mstari na kueka mbaazi kando ya mstari.