Kuandaa kitalu cha miche ya pilipili kunahitaji juhudi, lakini kuna manufaa. Kitalu kizuri husababisha mbegu zote kuota, na miche yote huwa na urefu sawa.
Anza na mbegu zenye ubora wa hali ya juu ambazo zinaweza kustahimili magonjwa. Ikiwa una shamba kidogo ambapo unataka kupanda, tumia trei. Kama una shamba kubwa, unaweza kuandaa kitalu shambani karibu na chanzo cha maji.
Andaa vizuri sehemu unapotaka kuweka kitalu. Fanya kitalu kiwe cha upana wa mita moja na urefu wowote. Sawazisha kitalu na umwagilie maji ya kutosha kabla ya kupanda. Chora mitaro ambayo huachana na umbali wa 15cm. Panda mbegu chache kwenye kila mtaro na kisha zifunike kwa udongo laini. Funika udongo na matandazo ili udongo ubaki na unyevu. Baada ya mbegu kuota, ondoa matandazo na ongeza mbolea kati ya safu ikiwa udongo ni duni. Kisha, tengeneza kivuli juu ya kitalu, lakini ondoa matandazo haya ukikurubia wakati wa kupandikiza ili miche iwe thabiti.
Mbinu nyigine
Changanya mbegu na mchanga kabla ya kupanda ili kuzitenganisha.
Ikiwa ukuzaji wako wa awali ulisumbiliwa na viini au nyugunyugu, tumia joto ili kudhibiti wadudu na magonjwa.