Lishe ya mchanganyiko hukithiri virutubisho, lakini ni ghali ikinunuliwa dukani. Kwa hivyo, kuandaa lishe ya mchanganyiko kwa kulisha wanyama wote inaweza kusaidia kuokoa muda na pesa.
Umuhimu wa lishe ya mchanganyiko kwa mifugo ni kwamba wanatoa maziwa na mayai zaidi. Pia husaidia wanyama na samaki kukua haraka na kuwa na nguvu.
Maandalizi ya mchanganyiko
Theluthi mbili ya mchanganyiko hufanywa kutoka kwa nafaka kama mpunga, mahindi, mtama na mawele. Kila kiungo huhifadhiwa pekee. Nafaka ni chanzo cha wanga, na huwapa wanyama nguvu. Mtama una fumuele mwingi, an pia huongeza harufu na ladha bora. Theluthi moja ya mchanganyiko inafaa kuwa na protini na mafuta. Saga mchanganyiko kuwa unga usiyolaini. Unga laini sana huingia kwenye mapafu ya wanyama. Kutumia unga laini katika samaki huzuia samaki waliyochini kupata chakula cha kutosha.
Kwa chakula cha ng‘ombe, kondoo na mbuzi, ongeza kiasi sawa cha wishwa wa ngano au mchele. Kwa kuku na samaki ongeza poda wa samaki iliyokaushwa. Mchanganyiko wa msingi unaweza kuhifadhiwa hadi miezi minne. Chakula kinaa kuhifadhiwa vizuri dhidi ya ardhi na unyevu.
Badala ya keki ya karanga unaweza kutumia keki ya nazi au ufuta. Samaki hawawezi kulishwa keki ya nazi, kwani ina mafuta mengi ambayo huelea juu ya maji, na vili vile kuzuia oksijeni kutolewa kwa samaki.