Madoa meusi ya bakteria (BBS) ni ugonjwa wa kuvu ambao huenea takribani mita 10-200 kwa mwaka. Ugonjwa huo hupunguza matawi na kusababisha kudondoka kwa matunda. Hatua ya kutumia mikono pamoja na kemikali kudhibiti ugonjwa hupunguza kuenea.
Ugonjwa huonyesha dalili vile vile kama za ugonjwa wa anthracnose, kwa hivyo unahitaji uangalifu mkubwa. BBS huenea zaidi kupitia vifaa vya upandaji vilivyoathiriwa, magari yanayotumika kwa kusafirisha, hali ya unyevu na tufani, na huathiri sana mavuno. Kwa hivyo, ugonjwa huo unahitaji hatua jumuishi ya kuudhibiti. Dalili za BBS: Vidonda vya manjano, madoa meusi kwenye majani, madoa meusi kwenye matunda, na matawi yaliyo na vidonda.
Kudhibiti BBS kwa mikono
Kagua shamba la embe mara kwa mara, ondoa maembe yaliyoshambuliwa na uyachome ili kupunguza uwezekano wa kueneza ugonjwa. Kwa kuongezea, kagua miti ya embe kwa kasoro, na upogoe na kuharibu mabaki. Kamwe, usifanye kazi shambani wakati wa mvua na wakati matawi yana unyevu ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa. Tumia spiriti na pombe kali kukinga vifaa dhidi ya viini baada ya kufanya kazi katika maeneo yaliyoathiriwa.
Kudhibiti BBS kwa kemikali
Nyunyizia BBS na viuakuvu. Soma maagizo ya kutumia kemikali, na wasiliana na wakulima wenzako kwa mchanganyiko unaofaa. Hata hivyo, badilisha kemikali unazotumia ili ugonjwa usigeuke sugu dhidi yazo.