Minyoo fundo ni minyoo ambayo hutambuliwa rahisi kwa; mimea kudumaa, na fundo la mizizi kwenye mboga. Minyoo fundo hawawezi kuuliwa na viuakuvu au viuawadudu kwasababu wanaishi kwenye mizizi chini ya udongo ambapo wanakamilishia mzunguko wa maisha yao.
Maisha ya minyoo fundo
Minyoo fundo hutaga mayai nje ya nundu za mizizi ambapo minyoo michanga huanguliwa na kuvamia mizizi kwa kutumia sehemu za mdomo zilizoelekezwa, kwa hivyo kupunguza uingizaji wa maji na virutubisho.
Hatua za kuzuia minyoo fundo
Panda miche yenye afya na sugu kutoka kwa wauzaji wanaoaminika. Ondoa mizizi yote kutoka kwenye kitalu na uichome, kisha weka samadi au mboji ili kurutubisha udongo. Zaidi ya hayo; haribu vyanzo vyote vya minyoo fundo, lima shamba lako na uache udongo ukiwa umepinduliwa ili kukaushwa na jua, ondoa magugu na ng‘oa mimea iliyoathiriwa ili kupunguza vyanzo vya chakula cha minyoo fundo. Hakikisha kwamba unakagua shamba mara kwa mara ili kuharibu mimea iliyoathiriwa, na vile vile kupanda aina tofauti ya mimea sugu kwa misimu kadha ili kuangamiza ugonjwa huo. Wakati wa kutoka shamba moja kwenda lingine, safisha vifaa vya shamba, na miguu vizuri. Mwishowe, punguza mtiririko kasi wa maji kwa kuunda matuta, na kupanda mimea mitego ili kuzuia kuenea kwa magonjwa.