Nyanya ni moja wapo ya mboga muhimu ambayo hulimwa ulimwenguni kote. Nyanya huliwa mbichi, au kupikwa kama chanzo kikuu cha vitamini, na madini.
Nyanya pia ni chanzo kizuri cha mapato kwa wakulima wengi.
Nyanya huathiriwa na wadudu wengi, na magonjwa. Bakajani chelewa ni ugonjwa haribifu.
Dalili za ugonjwa
Vidonda vyeusi vya majani ambavyo baadae hugeuka hudhurungi. Vidonda vya rangi ya hudhurungi vilivyo na majimaji hutokea juu ya matunda, na mwishowe mmea hufa.
Ugonjwa huo husababishwa na ukungu, na huenea kwa chembe za kuvu. Chembe za kuvu huhamishwa na upepo, maji ya mvua na maji machafu.
Usimamizi wa ugonjwa
Usipande mazao kama vile viazi, pilipili, biringani pamoja na nyanya kwa sababu wote huathiriwa na bakajani chelewa.
Ongeza mbolea au mboji, na chokaa ili kupunguza asidi.
Udhibiti wa ugonjwa
Panda aina sugu kama inavyoshauriwa na bwanashamba au mshauri.
Simamisha mimea ili isiguse ardhi.
Fanya ukaguzi wa kila siku shambani ili kugundua ukuepo wa ugonjwa.
Choma sehemu za mmea zilizoathiriwa. Usiweke sehemu za mmea mgonjwa kwenye mbolea.
Safisha zana au vifaa vilivyotumiwa, kwa sabuni au maji yaliyochemka ili kuua viini.
Pogoa mimea kwa kukata matawi ya chini.
Panda mimea tofuati kwa misimu tofauti ili kuangamiza mzunguko wa magonjwa.
Nyunyizia dawa ya kiasili na viuakuvu.