Linda mavuno ya mahindi dhidi ya kuungua kwa kuepuka ugonjwa wa tar spot .
Tar spot ni kuvu, ambayo husababisha hasara kubwa ya mavuno ya mahindi. Unaweza kuitambua, kwa madoa madogo meusi ambayo yanaonekana juu ya majani. Karibu na madoa meusi kuna matangazo mepesi ambao hufanana na jicho la samaki. Ugonjwa huo ukiendelea, majani yatote huungua. Kuungua huanzia chini ya mmea na kuendelea juu. Ugonjwa wa Tar spot husababisha gunzikuoza na ikiwa uharibifu ni mkubwa, nafaka huota mapema. Kuvu huo hushambulia mimea wakati gunzi ni ndogo hadi wakati nafaka hukua. Hii huepo kama siku 30 hadi 50 baada ya mimea kupandwa. Mmea mchanga huendelea kushambuliwa sana na kuvu kadiri unavyokuwa.
Hali ya hewa iliopoa na baridi
Ugonjwa husambaa katika hali ya hewa baridi. Hewa huleta unyevu wakati wa usiku na asubuhi mapema. Ugonjwa wa Tar spot husababisha uharibifu kila mwaka, ikiwa mabaki ya mahindi yaliyoshambuliwa hubaki shambani.
Kudhibiti ugonjwa watar spot
Ikiwa ulikuwa na dalili za madoa ya ugonjwa wa tar spot mwaka uliopita, ni bora kuchoma mabaki ya mazao. Katika sehemu nyingine unaweza kuanza kupanda mahindi mapema, ili kuepuka tar spot. Ili kudhibiti tar spot kusambaa juu ya ardhi, usipande mahindi kwenye shamba moja kila mwaka. Pia panda mmea mwingine kama maharagwe au mpupu. Tumia aina za kienyeji au aina ambazo ni sugu zaidi dhidi ya kuvu. Ikiwa ugonjwa unaonekana lakini majani bado yana afya, unaweza kunyunyiza dawa ya kuvu. Anza kunyunyizia dawa ya kuua kuvu mara tu utakapoona nukta ndogo za kwanza nyeusi. Ikiwa majani tayari yamechomwa, hapo basi dawa haina athari yote ya kudhibiti kuvu.