»Kudhibiti vidukari kwenye maharagwe na mboga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/managing-aphids-beans-and-vegetables

Muda: 

00:09:13
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

CCDB

Vidukari ni wadudu wadogo, rangi ya kijani au nyeusi. Vidukari huharibu mimea kwa kunyonya maji yake, kwa hivyo hukua polepole. Vidukari pia huhamisha magonjwa ya virusi.

Jinsi vidukari wanaishi

Vidukari huishi kwa makundi. Katika jua kali, vidukari huhamia chini ya majani ili kupata kibaridi. Vidukari wakikomaa,wengine hupata mabawa na huruka kwa mimea na mashamba mengine. Vidukari hutoa kinyesi kitamu. Kinyesi hiki huitwa utomvu. Mchwa hula utonvu, na pia hupatikana kwenye majani. Jivu husaidia kufanya majani kuwa magumu. Hivyo, vidukari hawawezi tena kunyonya maji kutoka kwa majani. Vidukari hushambulia sana maharage na mboga. Mazao mengine yanaoshambuliwa ni haradali, kabichi na jani la mtambu.

Kudhibiti vidukari

Tembelea shamba lako kila mara ili kutambua vidukari. Wangamize vidukari kwa vidole. Nyunyiza majivu poa asubuhi, ili umande ufanye majivu haya yashikamane na majani. Nyunyiza majivu ya mabua ya mpunga au kuni. Kamwe, usitumie majivu ya majani ya ndizi, maharadali, mianzi na majani ya miti, kwasaba majivu haya yana nguvu sana, na yatachoma mimea ya mboga.

Unaweza pia kutumia maji ya sabuni. Sugua sabuni kwenye tungi la maji hadi litakapotoa povu. Nyunyiza maji haya shambani mara moja kila siku, kwa siku 3. Tumia mchanganyiko wa mwarobaini ili kudhibiti vidukari. Saga kilo 2 za majani ya mwarobaini na uchanganye na lita 16 za maji. Nyunyiza mchanaganyiko huo mara moja kila siku kwa siku 3.

Panda ufuta na mimea ya maharadali karibu na shamba lako. Kwa hivyo, dudu kobe huvutiwa na kula vidukari.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:34Vidukari ni wadudu wadogo, rangi ya kijani au nyeusi. Vidukari mara nyingi hushambulia maharagwe na mboga.
00:3500:44Vidukari pia hushambulia mazao kama vile maharadali, kabichi na jani la mtambu.
00:4500:50Uharibifu hufanywa na vidukari kwa kufyonza utomvi wa mimea.
00:5100:59Vidukari huhamisha magonjwa ya virusi hadi kwenye mimea yenye afia
01:0001: 10Unaweza kudhibiti vidukari bila viuatilifu/ viuawadudu.
01:1101:34Vidukari huishi kwa makundi na hunyonya maji ya maua na matunda
01:3501:57Vidukari wana miili laini, na katika jua kali, vidukari huhamia chini ya majani
01:5802:19Vidukari huruka wakiwa wamekomaa. Kinyesi chao huvutia mchwa.
02:2002:25Jinsi ya kudhibiti vidukari.
02:2602:39Ukaguzi wa shamba mara kwa mara.
02:4003:24Wangamize vidukari kwa vidole
03:2504:50Nyunyiza majivu ya mabua ya mpunga au kuni.
04:5105:42Unaweza kunyunyiza pia maji ya sabuni.
05:4306:21Tumia mchanganyiko wa mwarobaini.
06:2206:48Tumia dudu kobe.
06:4907:39Panda ufuta na mimea ya maharadali karibu na shamba
07:4009:13Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *