Mpapai ni mti wa kudumu na una thamani ya lishe na dawa. Mpapai hauwezi kustahimili ukame kwa muda mrefu.
Papai hustawi katika maeneo ya joto nyuzi hadi 20–30, katika udongo tifutifu ambao una maji ya kutosha na mboji. Mbegu zinaweza kupandwa moja kwa moja shambani au kwenye kitalu, viriba vya plastiki au vyombo. Utunzaji wa miche kwa uangalifu ni muhimu ili kuzuia kuathiri mizizi.
Upandaji wa mipapai
Udongo ulio kwenye kiriba cha platiki unahitaji kuwa na mboji ya kutosha, uchanganywe na samadi, na mbolea ya NPK ili kuongeza rutuba ya udongo.
Chimba mashimo ya upana wa sm 60 kwa urefu wa sm 60, na muachano wa mita 3. Baada ya kuchimba mashimo, tenganisha theluthi ya udongo wa juu na theluthui wa udongo wa chini.
Kuongeza mbolea
Changanya mbolea na udongo wa juu na uurudishe kwenye shimo.
Weka mche katikati ya shimo na ufunike miche kwa uthabiti. Mwagilia maji wakati wa asubuhi na jioni.
Panda mazao mengine kama vile maharagwe ambayo huongeza nitrojeni kwenye udongo. Maharage huunda matawi ambayo hupunguza gharama ya kupalilia. Kila mwezi, ongeza mbolea ya NPK na mbolea ya majani kudhibiti upungufu wa madini na magonjwa.
Kuvuna papa
Mipapai huanza kutoa maua miezi 5–8 baada ya kupandwa, na huwa tayari kuvunwa takribani miezi miwili baada ya hatua ya kuchanua maua.
Mapapai huwa yamekomaa yanapoanza kugeuka manjano. Wakati wa kuvuna, pindua papai ili kuikata au tumia kisu.