Kugeuza taka za samaki kuwa mbolea

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/turning-fish-waste-fertiliser

Muda: 

00:15:20
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Access Agriculture
Rutuba ya udongo ni jambo muhimu ambalo huamua tija ya ardhi, na inaweza kuboreshwa kwa kutumia mbinu sahihi za kilimo.
Utumiaji mwingi wa mbolea za kemikali huharibu afya ya udongo, jambo ambalo hupungunza tija yake, na hilo linaweza kuboreshwa kwa kutumia nyenzo asili. Takataka za samaki ni sehemu za samaki ambazo watu hawali, na hizi zimekithiri Nitrojeni, fosforasi, kalsiamu na vitamini..

Kutengeneza wa mbolea

Ili kutengeneza mbolea ya maji ya samaki, chachusha taka za samaki kwanza.Kata taka za samaki katika vipande vidogo ili kuharakisha uchachushaji na vaa glavu ili kuepuka majeraha. Viumbe hai ambavyo huchachusha taka huhitaji sukari kukua, kwa hivyo ongeza kilo 3 za sukari au molasi na uchanganye vizuri.
Vile vile, weka mchanganyiko huo kwenye ndoo ya plastiki, uifunike kwa kifuniko kisichopitisha hewa na uiweke kwenye kivuli. Kisha koroga mchanganyiko mara moja kwa siku na, mchanganyiko utakuwa tayari baada ya wiki 4. Chuja mchanganyiko kwa kitambaa cha pamba, na uweke mchanganyiko mahali pa giza.
Ili kutumia mbolea ya maji, yeyusha kwanza na kunyunyizia kwa mboga za majani na nafaka.  Changanya lita 10 ya maji na lita 1 ya mbolea. Nyunyizia mimea mara mbili, yaani, wakati mmea ukiwa mchanga na wakati wa kutoa maua. Kwa mazao ya miti, changanya lita 2 za mbolea na lita 10 za maji na nyunyizia mmea wakati wa kuchanua maua na baada ya kuvuna.
Ili kutengeneza mbolea ya samaki ya udongo, chimba shimo la kina cha nusu mita na ukubwa kadhaa kulingana na wingi wa mbolea inayohitajika. Shimo lazima lichimbwe chini ya kivuli. Kata taka katika vipande vidogo, vichanganye na kilo 5 za sukari na ongeza kilo 65 za samadi ya ng’ombe iliyooza vizuri.  Hamisha mchanganyiko kwenye shimo na lifunike na majani mapana hadi kina cha 1cm, mbolea itakuwa tayari baada ya miezi 2.
Baada ya kulima mara ya mwisho, weka kilo 20 za mbolea hii iliyochanganywa na kilo 10 za samadi ya ng’ombe juu ya udongo. Hatimaye, weka mbolea kwenye mimea na miti mara moja baada ya kila baada ya miezi 3.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:22Utumiaji mwingi wa mbolea za madini huharibu afya ya udongo.
00:2300:38Afya ya udongo inaweza kuboreshwa kwa kutumia rasilimali asilia.
00:3901:58Takataka za samaki ni sehemu za samaki ambayo watu hawali.
01:5903:06Kwa mbolea ya maji ya samaki, chachusha taka ya samaki kwanza.
03:0704:10Kata taka katika vipande vidogo na ongeza sukari au molasi na kuchanganya vizuri.
04:1104:53Weka mchanganyiko huo kwenye ndoo ya plastiki, uifunike na uiweke kwenye kivuli.
04:5405:35 koroga mchanganyiko mara moja kwa siku na, mchanganyiko utakuwa tayari baada ya wiki 4.
05:3605:44Chuja mchanganyiko kwa kitambaa cha pamba
05:4506:25 Weka mchanganyiko mahali pa giza
06:2606:35Changanya maji na mbolea ili kunyunyizia mboga na nafaka.
06:3608:00 Nyunyizia mimea kabla ya kuweka matandazo na pia kwenye miti.
08:0108:23Chimba shimo kulingana na wingi wa mbolea inayohitajika.
08:2409:31Kata taka katika vipande vidogo, vichanganye na sukari na samadi ya ng'ombe iliyooza.
09:3211:02Hamisha mchanganyiko kwenye shimo na lifunike na majani mapana hadi kina cha 1cm, mbolea itakuwa tayari baada ya miezi 2.
11:0315:20Baada ya kulima mara ya mwisho, weka mbolea hii iliyochanganywa na samadi ya ng'ombe juu ya udongo.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *