Upandaji endelevu wa mazao pamoja na miti huongeza tija ya ardhi katika kipindi fulani, jambo ambalo huboresha kipato cha mkulima.
Ingawa mfumo wa kilimo mseto unavyosababisha mavuno mengi pamoja na uwezekano bora wa kiuchumi, uwekezaji wa awali kwa ujumla ni wa juu zaidi.
Utunzaji wa mandhari
Kwa kuwa na ustahimilivu pamoja na uwezo wa kuzalisha kwa muda mrefu, mazao ya kudumu huongeza mapato kwa mwaka mzima, na mizizi yake huboresha afya ya udongo. Mizizi ya miti hulinda ardhi dhidi ya mmomonyoko, majani yake huboresha mboji na pia miti huwezesha maji kupenyeza udongo pamoja na kuhifadhiwa vizuri udongoni.
Vile vile hupunguza uvukizi, na huboresha hali ya hewa katika mashamba. Mimea ya jamii ya kunde hutengeneza na kutolea mimea mingine nitrojeni. Mfumo jumuishi wa kahawa na kakao una vichavushaji zaidi na viumbe-hai vyenye manufaa ambavyo hudhibiti wadudu na magonjwa. Ikiwa msongamano wa upandaji ni wa juu sana, unyevu unaotokea unaweza kusababisha magonjwa ya ukungu.
Zaidi ya hayo, ugumu wa utekelezaji wa kilimo mseto huhitaji ujuzi zaidi wa kitaalamu, kazi zaidi, ubunifu na kufanya maamuzi sahihi. Ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kunahitaji juhudi za pamoja, kuimarisha kilimo hai na kupunguza ukataji ovyo miti.
Hatimaye, jumuisha kilimo mseto na unganisha matumizi sahihi ya ardhi na maeneo yenye thamani kubwa ya kiikolojia ili kufikia mfumo endelevu wa chakula unaostahimili zaidi.