Kufuga kware ni maarufu zaidi kwa wakulima kwa sababu mayai yao yana lishe zaidi, vitamini B1 na B2 na madini kuliko mayai ya kuku.
Kware ni ndege walio kwenye hali ya hatari, kwa hivyo wanahitaji makazi bora. Kizimba kizuri cha kware huhakikisha ulinzi wao.
Faida za ufugaji wa kware
Kware ni rahisi kufuga kwani wanakula kidogo na hawapati magonjwa mara nyingi. Kware hukua haraka na huanza kutaga mayai wakiwa na umri wa wiki 6. Kware ni wadogo kwa ukubwa, na wanaweza kukuzwa katika nafasi ndogo.
Mahitaji
Vifaa vya ujenzi vinaweza kupatikana kutoka duka la vifaa. Kizimba kinachopendekezwa kwa kila ndege 20 kinafaa kuwa na: urefu wa 2 ft, upana wa 2 ft, kina cha 4 ft juu kutoka kwa sakafu. Vifaa ni: 2m bati la chuma, mbao laini (plywood), mbao ya futi 90 iliyo na mita 2 kwa 2. Mbao ya futi 80 iliyo na mita 2 kwa 1, futi 30 za wavu uliyo na 1/2 inchi, misumari na jozi 2 za bawaba zilizo na inchi 3.
Ujenzi wa chumba cha kware
Kware wanahitaji kulindwa kutokana na mvua, na joto. Wanafaa kupata hewa safi. Kware huhitaji chumba cha kuwachunga dhidi ya paka na umbwa kwa sababu wao hutawanyika sana kwa pande zote.
Fremu ya kizimba hujengwa kwa kutumia mbao. Mbao laini (plywood) hukatwa ili kutengeneza sakafu, na kuwezesha kusafisha rahisi, na pia kuzuia kware kutokwama. Kwa pande, nyavu zinabandikwa ili kuhakikisha mzunguko mzuri wa hewa. milango na miguu hujengwa na kuwekwa kwenye kizimba. Makaazi sahihi ya kware huhakikisha ulinzi mzuri unaokusaidia kupata faida kubwa.