Kahawa zao la kudumu ambalo tija yake hupungua baada ya muda, na hivyo kukata mashina mazee ni muhimu.
Ili kukata mashina ya mibuni mizee, tumia kisu cha kupogolea badala ya panga. Huku kunafanywa wakati mbuni umetimiza kati ya miaka 7 hadi 9, wakati ambapo tija ya kahawa imepungua. Hata hivyo, usikate mashina wakati wa kiangazi bali katika msimu wa mvua kwa sababu mibuni inaweza kukauka.
Steps involved
Usikate mashina machanga yenye afya, bali kata mashina kubwa yaliyokomaa.
Wakati wa kukata mashina, pima futi moja kutoka ardhini na ukate shina kwa pembe ya digrii 45. Huku husaidia kutiririsha maji yanayotoka kwenye kisiki, ambayo yangeweza kusababisha shina kuoza yanapotwama juu ya kisiki, na vile vile kusababisha mmea mzima kufa.
Kukata mashina husaidia kahawa kuzaa matunda zaidi kuliko mara ya awali.
Baada ya mwaka mmoja, mashina mapya huanza kutoa matunda ya kahawa.