Kukausha huwezesha wakulima na wauzaji wa mboga kupunguza hasara, na kuuza mboga za majani nje ya msimu wa uvunaji kwa sababu mboga huharibika haraka siku kadha baada ya kuvuna.
Majani ya sukumawiki yaliyokaushwa vizuri hutoa sauti ya kupasuka wakati yanaguswa, lakini majani yaliyokaushwa sana hugeuka hudhurungi na hii hupunguza ubora wake.
Mchakato wa kukausha
Vuna majani mabichi, toa wadudu na uchafu. Hata hivyo usivune majani ya juu kabisa, ili mmea uendelee kukua. Safisha mikono kwa sabuni na maji safi, chambua ili kutenga majani mazuri na uondoe mabua kwa sabubu ni magumu kula. Kisha, safisha majani mara mbili katika maji safi ili kuondoa wadudu na uchafu.
Lowesha majani kwenye maji ya vuguvugu yaliyo na chumvi ili kuyalainisha, na kisha koroga kuhakikisha kwamba kila jani limepata chumvi vizuri. Usichemshe maji yatokote, kwasababu majani yatapoteza lishe au madini. Kisha, weka majani kwenye maji baridi ili kuyahuhisha upya. Weka majani kwenye waavu uliyoinuliwa ili maji yadondoke, na kisha yasambaze kwa kikaushaji cha jua ili yakauke.
Baada ya siku 2, kagua kama majani yamekauka vizuri kwa kuyagusa ili yatoe sauti kavu. Weka majani kwenye mifuko ya plastiki na uifunge. kisha weka mifuko hiyo kwenye chombo kisicho penyeza hewa ili kuzuia vumbi, unyevu na kwa ulinzi zaidi. Mwishowe, hifadhi chombo hiki kilicho na sukumawiki kwenye chumba safi, kisichopenyeza jua moja kwa moja.