Usindikaji wa zao
Kwanza, weka nanasi kwenye kivuli, zichambue, zipime na zioshe, zisuuze, na kisha ziache zikauke. Watu wenye afya njema wenye kucha fupi na mikono safi ndio wanapaswa kushughulikia nanasi. Wanapaswa kumenya mananasi na kuondoa macho yote na kuzikata katika maumbo yanayotakiwa katika vipande vya unene wa unusu sentimita.
Vile vile, tandaza vipande kwenye trei ili vikauke sawasawa, na weka trei kwenye kikaushio na ukifunge vizuri ili kudumisha joto linalofaa, pamoja na kuzuia wadudu na vumbi kuingiza. Mananasi hukauka kwa siku 2 na kuondolewa na kupozwa kabla ya kufungashwa.
Fungasha mananasi kwenye chombo kikubwa kisichopitisha hewa, na hatimaye chambua, pima na panga mananasi kulingana na uzito unaohitajika sokoni.