Kwa kuwa ni mboga muhimu na yenye lishe bora, ubora na wingi wa biringanya huamuliwa na teknolojia inayotumika katika uzalishaji wake.
Upandaji wa mbiringanya hutekelezwa kwa kuhamisha miche kutoka kwenye kitalu. Miche hupandikizwa siku 45–50 baada ya mbegu kupandwa, na wakati ambapo mche una majani 4–6 na urefu wa cm 10–12.
Usimamizi wa mbiringanya
Kabla ya kupanda, mashimo huchimbwa udongoni na mara tu miche inapowekwa, hufunikwa na kumwagiliwa maji. Mpangilio wa upanzi hufanywa kulingana na mahitaji ya aina itakayopandwa, na idadi ya mashina yatakayoachwa shambani.
Mwanzoni mwa uundaji wa matunda, mfumo wa umwagiliaji huwekwa mbali na mmea ili kudhibiti upenyezaji wa mizizi ardhini kwa kina kirefu, jambo ambalo husitisha ukuaji wa majani, na vile vile huathiri utoaji na urutubishaji wa maua. Kupogoa hufanywa siku 40–50 baada ya kupanda, huku mashina 2–3 au 4 yakiachwa kwenye mmea. Vijiti husimikwa ardhini ili kusimamisha wima mimea na kuboresha uingizaji wa hewa kwenye mimea.
Vile vile, ondoa majani ya ziada ili kuboresha rangi ya matunda na uingizaji wa hewa. Ondoa matunda yote yaliyoathiriwa na magonjwa. Maua ya kwanza huonekana siku 20–30 baada ya kupandikiza na katika hali hii, mizinga ya nyuki huwekwa kwenye chafu ili kuboresha uchavushaji wa maua.
Baada ya kurutubishwa, matunda hutokea na hivyo umwagiliaji wa maji hutekelezwa kulingana na mahitaji ya mazao, na kiwango cha uvukizaji. Chukua tahadharini na kiasi cha mbolea ya Nitrojeni kitakachotumika ili kuepuka ukuaji wa majani ya ziada.
Inzi weupe na chawa ndio wadudu waharibifu sana wa zao la biringanya. Hata hivyo, kuna njia maalum ya udhibiti wa kibayolojia dhidi ya wadudu waharibifu. Kipindi cha ukuaji kutoka hatua ya kuchanua maua hadi kuvuna ni kati ya siku 10–40 kulingana na aina ya biringanya, na halijoto.
Hatimaye, uvunaji wa matunda hufanywa kabla ya matunda kufikia ukomavu wa kifisiolojia. Matunda huchunguzwa kwa unyevu asubuhi na vifaa vya kupogolea hutumika kuvuna ili kuzuia kuharibu matunda. Hakikisha kwamba unaacha kijiti ambacho hushikilia tunda cha urefu wa 1cm wakati wa kuvuna.