Mananasi yanahitajika sana, na yanapendekeza halijoto la nyuzi joto 21 – 29 Celsius na mvua wa wa wasitani wa takribani 600mm. Kujifunza mapendekezo yao ya ukuaji husaidia kuongeza uzalishaji.
Panda kwenye mteremko tambarare kwa ajili ya kuondoa maji ya ziada shambani. Fanya kilimo cha mzunguko wa mazao. Pumzisha na usilime shamba kwa miaka 3. Haya husaidia kudhibiti magugu, wadudu na magonjwa. Uzito wa mbegu (chipukizi) unaokubalika ni kati ya 250 – 450 gramu.
Mapendekezo ya ukuaji
Chagua eneo lililo karibu na barabara kwa usafirishaji rahisi wa pembejeo na mazao hadi sokoni. Pia shamba la mananasi lazima liwe karibu na chanzo cha maji cha kudumu kwani maji ni muhimu kwa shughuli za shamba. Tayarisha ardhi kwa kufyeka, kuchoma na uondoe mashina na mizizi ya miti ili kutunza rutuba ya udongo. Lima shamba mara 2 baada ya muda wa wiki 3 huku ukichanganya udongo mara 2 ili kuruhusu uozo. Tengeneza mitaro yenye upana wa sm 60– 70, urefu wa sm 30 na muachano wa 50 – 60 kati yao ili kudhibiti magugu. Sawazisha uso wa mitaro ili kuzuia mkusanyiko wa maji ambayo yanaweza kusababisha magonjwa ukungu.
Kuweka mbolea
Weka mbolea za mono ammoniamu, salfa ya amonia na urea kwenye mtaro ili kuimarisha rutuba ya udongo. Funika matuta kwa matandazo ya plastiki nyeusi ili kuhifadhi unyevu na kudhibiti magugu. Gueuza mbegu ili sehemu ya chini iangalie juu, kisha weke mbegu juu ya mimea mama na ili mbegu zipate mwanga wa jua. Kata na upunguze baadhi ya sehemu za mbegu. Ondoa mbegu zilizo na magonjwa, na majani ya chini ili kuhimiza ukuzaji wa mizizi na pia kudhihirisha wadudu wanaojificha kama vile matekenya na mchwa. Kabla ya kupanda tibu mbegu kwa dawa iliyopendekezwa. Mwishowe panda kwa sentimita 30 kati ya safu na cm 25 kati ya mimea kwa ukuaji mzuri wa mizizi.