Kwa kuwa ni zao muhimu lenye lishe, tikitimaji hulimwa sana kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo, mbinu za usimamizi wake hazitekelezwi kikamilifu na wakulima, jambo ambalo hupunguza ubora na wingi wake.
Upapopanda tikitimaji, panda mbegu kwenye vitalu. Pandikiza katika wiki 6–7 baada ya kupanda wakati jani la kwanza linapokua vyema. Hata hivyo, ni bora kupandikiza kama majani 2 yamekua kikamilifu, na jani la 3 au la 4 linaonekana.
Hatua za usimamizi
Wakati wa kupanda, tengeneza mashimo, weka miche ndani na funika mizizi kwa udongo, kisha mwagilia maji. Weka matandazo ili kuongeza joto la udongo, kupunguza uvukizi, kupunguza ukuaji wa magugu na kuongeza ubora wa matunda kwa kuzuia mgusano wa moja kwa moja na udongo. Unaweza kutandaza udongo kwa kutumia damani nyeusi ya plastiki.
Baada ya kupanda, weka mitaro ya plastiki ili kuongeza viwango vya joto. Njia ya kufunika miche ndani ya damani ya plastiki pia hutumiwa kuongeza joto, kuboresha uingizaji wa hewa na kuzuia matatzio yanayohusiana na umwagiliaji wa njia ya matone.
Simamisha mimea ili kuzalisha tikitimaji bora. Acha umbali wa mita moja ya mraba kwa mimea 0.75 hadi 1 iwapo unapanda mimea inayotambaa, huku ukiacha umbali wa mita moja ya mraba kwa mimea 1.5 hadi 2 unapopanda mimea inayosimamishwa. Pogoa mimea ili kuhimiza ukuaji wa matawi na huharakisha ukuaji, pamoja na kuongeza ubora na ukubwa wa matunda.
Njia ya umwagiliaji inayopendekezwa ni umwagiliaji kwa njia ya matone kwani tikitimaji huathiriwa ma maji mengi sana. Uchavushaji hufanywa na nyuki, kwa hivyo weka mizinga ya nyuki shambani siku chache kabla ya maua ya kike kuonekana, na baada ya maua ya kiume kwanza ya kutokea.
Maua hutokea kwa hatua ili kutoa nafasi kwa mmea kuzaa matunda 3 hadi 4. Maua hubaki yamejifungua kwa siku 2–3, kwani hujifungua asubuhi na hujifunga jioni. Inachukua siku 100–120 kutoka mwanzo wa ukuaji wa mmea hadi mwanzo wa kuvuna. Hii husababisha utoaji wa matunda kutofautiana kati ya siku 30 hadi 50, kulingana na aina ya mmea, na mazingira ya ukuaji.
Hatimaye, matunda hayavunwi hadi yatakayokomaa, na uvunaji hufanywa kwa kutumia mkono. Mara ya kuvuna tofautiana kutoka mara 2–3 kwa wiki wakati wa hali ya hewa ya joto au mara moja wakati wa baridi.