Mihogo ni chanzo cha chakula, hata hivyo maji ya mvua husomba udongo wenye rutuba na mavuno ya muhogo hupunguka. Mavuno mazuri ya muhogo yanahitaji kupunguza mmomonyoko wa udongo, na kutunza ardhi yenye afya.
Kwanza, panga mabaki ya mimea kwa muachano ya sentimita 20 kwa mistari ya upinde (contour lines). Panda safu ya nyasi, na jamii ya kunde ili kupunguza mtiririko wa maji ya mvua. Hii husaidia maji kupenyeza na kuacha udongo na virutubisho vilivyosombwa. Pia chimba miinuko au matuta kwenye maeneo yasiyo na bonde sana ili kuboresha jinsi maji yanavyopenyeza ardhini. Weka mbolea ya kikaboni ili kuboresha uzalishaji na rutuba ya udongo. Chimba mashimo ya kupanda ukifata contour kwa muachano wa mita 1. Nafasi hiyo inaweza kupunguzwa ikiwa udongo ni duni sana.
Nitrojeni, Fosforasi na Potasiamu
Unaweza kuongeza virutubisho kwa kutumia samadi au mbolea chache kwa ukuaji bora wa muhogo. Lakini usiweke samadi mbichi juu ya udongo, kwani inaweza kuyeyuka na kusombwa na maji kwa urahisi. Tumia pia N, P, K katika kila shimo la kupanda, kando ya samadi ili kuongeza mavuno. Katakata mashina ya aina bora za mihogo ambazo hutoa majani mengi, kwa urefu wa cm 15 – 20. Weka kila shina katika shimo huku sehemu za macho zikiangalia juu, na sehemu za chini zikiwa kwenye samadi.
Kilimo mseto
Wakati wa miezi 2–3 baada ya kupanda, weka nitrojeni au potasiamu kwani ndivyo virutubisho muhimu kwa muhogo unaokua. Walakini, usiweke mbolea ya madini wakati wa mvua na hali ya kiangazi kirefu ili kuepuka upotezaji wa virutubisho. Panda mimea inayokua kwa haraka ndani ya mihogo ili kulinda udongo dhidi ya magugu, kuongeza kiwango cha nitrojeni kwenye udongo, na kupunguza kazi ya kupalilia. Hakikisha kwamba unajadiliana na wakulima wengine juu ya hatua za kuboresha rutuba ya udongo.